Monday, October 14, 2013

Mahojiano na wadau wa darasa la Kiswahili Washington DC

Photo Credits: Panafricanvisions.com
Kiswahili inaaminika kuwa lugha asili ya Afrika inayozungumzwa na watu wengi kusini mwa jangwa la sahara.
Kama tunavyojua, ni lugha ya taifa kwa nchi za Tanzania naKenya, na pia yazungumzwa kwenye nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi, Rwanda, Uganda na visiwa vya Comoro.
Ikizungumzwa na watu wanaokadiriwa kufikia milioni 100 hivi sasa, Kiswahili ndio lugha pekee ya kiAfrika iliyo miongoni mwa lugha rasmi za Umoja wa Afrika. Na inaaminika kuwa lugha ya saba kwa watumiaji wengi duniani
Na matumizi yake kama lugha inayozungumzwa na wengi wenye lugha tofauti katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaifanya lugha hii kuwa muhimu zaidi kwa watu wengi walio na mahusiano na / ama wanaotaka kujishughulisha na biashara, kazi ama diplomasia katika ukanda huo.
Kiswahili sasa kinafunzwa katika vyuo visivyopungua 50 hapa nchini Marekani, lakini pia inafundishwa kwenye vyuo vikuu mbalimbali Ulaya na hata bara Asia.
Kiswahili ni lugha muhimu katika habari, shule, kazi za kiofisi, kidiplomasia na hata usalama miongoni mwa mataifa na naamini ndio sababu hata jumuiya ya waTanzania hapa Washington DC wakaona ni jambo la busara kuanzisha darasa la kufunza Kiswahili kwa watoto hapa DMV.
Na leo, wawakilishi wa wahusika wa mpango huo, Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Idd Sandaly pamoja na walimu Asha Nyang'anyi na Bernadeta Kaiza wamekuwa wakarimu sana kujiunga nami katika studio za JAMII PRODUCTION hapa Washington DC.
KARIBU UUNGANE NASI
Rais wa Jumuiya ya waTanzania DMV (Washington DC, Maryland na Virginia) Iddi Sandaly akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Bernadeta Kaiza ndani ya studio za Jamii Production
Mmoja wa walimu wa darasa la Kiswahili hapa Washington DC Asha Nyang'anyi akishiriki kipindi ndani ya studio za Jamii Production
Twawapenda....Tukutane juma lijalo kwa kipindi kingine cha HUYU NA YULE tutakapohojiana na wadau wengine juu ya jambo jingine MUHIMU kwa jamii yetu

No comments: