Monday, October 14, 2013

Mahojiano ya Jamii Production na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Dr Charles Kimei


Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei (kulia) akizungumza na Jamii Production  ndani ya ofisi ya Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico uliopo Jijini Washington DC
Jumatano ya Oktoba 9, 2013, Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRBD Dr Charles Kimei akiambatana na Mkurugenzi wa Masoko wa (CRDB) Tully Mwambapa, Bw. Mkurugenzi wa Hazina (CRDB) Alex Ngusaru na Msaidizi wa Dk.Kimei , Kenneth Kasigila walikuwa jijini Washington DC (pamoja na mambo mengine) kueleza mipango ambayo CRDB inayo katika kuboresha huduma za akaunti ya Tanzanite pamoja na kutambulisha huduma mpya ya JIJENGE.
Jamii Production ilipata fursa ya kuhojiana na Dr Kimei ambaye amefafanua mengi kuhusu huduma hizo.
KARIBU UUNGANE NASI

Na hapa chini ni mahojiano hayo katika SAUTI (AUDIO)
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei na akipata picha na mpiga picha mkuu wa Jamii Production Abou Shatry baada ya mahojiano.

No comments: