Wednesday, October 23, 2013

FIKRANI: "Injinia" MIMI na ukarabati wa "nyumba TANZANIA"


PHOTO CREDITS: Cool fun pics
".....Ni LAZIMA tuubomoe msingi wa nchi, kisha tuijenge upya.
MIMI na WEWE tuna wajibu mmoja. Kujua ni vipi tutaweza kuibomoa nchi sasa bila kuathiri "watu na mali" zilizo ndani kwani tusipofanya hivyo, "mali na watu" hao wataangukiwa na kuta na kuwa hasara zaidi mbele.
TUCHUKUE HATUA....HATUA SAHIHI...HATUA MAKINI.
  • Tukibomoa kwa umakini, tutapunguza gharama na hata baadhi ya vifaa vya ujenzi vitaweza kutumika tena.
  • Tusisubiri MJENZI aliyeijenga kwa makosa atuambie kuwa alikosea. Lakini tusimpuuze na kutomshirikisha kwenye ukarabati huu.
  • Tusimtishe kuwa tutamfunga kwa makosa ya ujenzi wake lakini tuhakikishe kuwa anajua kosa lake na halirudii tena.
  • Tusitafute sifa kwa kumshutumu mjenzi wa sasa na kusahau kutafuta SIFA ZA ATAKAYEKARABATI...."

***"FIKRANI" ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia.
Hiki kitakuwa kikikuletea habari na / ama mawazo mbalimbali yajayo fikrani mwangu kuhusu mambo mbalimbali maishani.
Mawazo tu........pengine...MAWAZO YA SAUTI

No comments: