Wednesday, October 23, 2013

FIKRANI: Uswahili, Mswahili na Kiswahili...Ni nini nani na kipi?


"...Siwezi kupinga kilichonifanya kuitwa MSWAHILI, kwa kuwa nilijua fikra za walioniita MSWAHILI.
Kwao waliamini kuwa kuongea kwa namna fulani ama hata kusikiliza miziki yenye mafumbo ama lugha fulani ni uswahili.
Na mimi nilikuwa natimia kwenye tafsiri yao.
Nilipenda na bado napenda maongezi yenye kueleza kitu kwa namna ya kibunifu.
Nilipenda na bado napenda maongezi ambayo yana mifano na kuchangamsha akili.
Nilipenda na bado napenda maongezi ambayo yana TUNGO TATA...."

***"FIKRANI" ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia.
Hiki kitakuwa kikikuletea habari na / ama mawazo mbalimbali yajayo fikrani mwangu kuhusu mambo mbalimbali maishani.
Mawazo tu........pengine...MAWAZO YA SAUTI

No comments: