Sunday, October 6, 2013

Kipindi maalum kuhusu tukio la ugaidi Westgate Mall nchini Kenya




Septemba 21 ilianza kama siku ya kawaida kwa waKenya wengi
Ilikuwa ni siku ya mwisho wa wiki, na kama ilivyo kwa siku nyingine kama hizo, pilika za mauzo na manunuzi zilikuwa zikiendelea ndani ya Westgate Shopping Mall jijini Nairobi.
Lakini hayo yalibadilika baada ya wavamizi kuingia humo na kuanza kufanya mauaji ya halaiki ambayo yalisababisha mapigano baina ya wapiganaji hao na jeshi la Kenya.
Mapigano yaliyodumu kwa siku nne na kusababisha vifo zaidi ya 70, kujeruhi zaidi ya watu 200 na mpaka sasa inasemekana makumi ya watu hawajulikani walipo.
Kujua zaidi kuhusu mtazamo wa JAMII juu ya kilichotokea, kinachotokea na (pengine) kinachotegemewa kutokea, naungana na wanaharakati wa kiKenya waishio hapa Washington DC Metropolitan kujadili hili.
Karibu uungane nasi 

Muendeshaji kipindi "KITINI"
Moja kati ya wanaharakati wa Jumuiya ya waKenya DMV na pia  Mtangazaji wa KIPINDI HIKI CHA ONE MIC SHOW (kitembelee hapa) Washington DC  Ali Badawy akiwa makini katika kipindi ndani ya Studio ya Jamii Production, Washaington DCni 
 Mwanaharakati mwingine, ambaye pia ni mtangazaji wa KENYA ONLINE RADIO (itembelee hapa) Mwalimu Mkawasi Mcharo Hall akiwa makini katika kipindi ndani ya Studio ya Jamii Production iliopo Washaington DC nchini Marekani.
Wanaharakati wa Jumuiya ya waKenya DMV Mwalimu Mkawasi Mcharo Hall alipokua akufanya mahojiano na Jamii Production kuhusu shambulio la mauwaji ya Westgate Mall  siku ya Jumamosi Sept 29 ndani ya Westgate Mall jijini Nairobi Kenya.

No comments: