JAMII tuliyonayo sasa ni matokeo ya wazazi na walezi waliotangulia.
Na...
Jamii tutakayokuwa nayo, itatokana na wazazi na walezi wa sasa (ambao ni kila mtu)
Ukweli ni kuwa..
DUNIA INABADILIKA. Na waliomo pia
Je!
Kuna tofauti gani (chanya na hasi) katika MALEZI ya zamani na sasa? Na vipi kuhusu malezi ya Afrika Mashariki na Tanzania?
Na ni nini kinaweza kufanyika kuboresha kizazi kijacho kwa kulea vema zaidi watoto wa sasa?
Unadhani malezi yetu ya sasa yanaendana na namna tunavyotaka wanetu wakue?
UNGANA NASI KATIKA KIPINDI HIKI CHA FAMILIA kujua zaidi
Mtayarishaji na Mtangazaji wa kipindi cha FAMILIA Dada Ndeletwa C. Lema akifurahia jambo wakati wa kipindi katika Studio za Jamii Production, Washington DC.
Mmoja wa wachangiaji wa kipindi cha FAMILIA Mama Martha akisikiliza kwa makini mchango katika mada iliyohusu jitihada za malezi ya watoto ndani ya familia zetu, kilichotayarisha na Dada Ndeletwa C. Lema ndani ya Studio ya Jamii Production.
Mmoja wa wachangiaji wa kipindi cha Familia Dada Oliver Lyimo, akichangia na kusikiliza mada inayohusu malezi ya watoto ndani ya familia zetu, kilichotayarisha na Dada Ndeletwa C. Lema ndani ya Studio ya Jamii Production.
No comments:
Post a Comment