Friday, October 25, 2013

WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON, DC

Mhe. Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akilakiwa na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga(kulia) wakati alipowasili Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Alhamisi Oct 24, 2013 kati ni Katibu wake Bwn. Juma Mswadiku
Picha zote kwa hisani ya Vijimambo Blog
 Mhe. Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
Mhe. Waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Dkt Fenella Mukangara akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Balozi Watanzania nchini Marekani Mhe. Mulamula na Afisa Habari wa Ubalozi, Mindi Kasiga wakiangalia.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwaongoza wageni wake Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara na Katibu wake kwenda kukutana na Maafisa wa Ubalozi kwenye ukumbi wa mikutano wa kumbukumbu ya Mwl. Julius Nyerere.
 Mhe. Liberata Mulamula, Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico akimkaribisha rasmi Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kufanya Utamburisho kwa Maafisa Ubalozi kujitamburisha kwa Mhe. Waziri kwa kutaja majina yao na nafasi zao za kazi kwenye Ubalozi huo.
 Maafisa Ubalozi wakimsikiliza Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakati alipokua akimtamburisha Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara  kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwl. Julius Nyerere
 Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara akiongea na Maafisa wa Ubalozi akiwapa salamu kutoka Tanzania na kuwaeleza mambo mbalimbali yanayoikabili nchini yetu yakiwemo swala la wahamiaji haramu na jinsi gani serikali inavyokabiliana nalo, swala lingine ni kuhusu ajira kwa Vijana, juhudi anazofanya kuwaelimisha Vijana jinsi ya kujiajiri wenyewe na pia alizungumuzia sekta binafsi kama zikifanya vizuri zitasaidia sana maendeleo ya nchi yetu na kutilia msisitizo swala la michezo mashuleni pia alielezea maswala ya vyombo vya habari na mchakato wa rasimu ya katiba unavyoendelea hizi sasa Tanzania. Baada ya maelezo ya Mhe. Waziri kulikuwa na kipindi cha maswali na majibu na kuchangia hoja mbalimbali kuhusu maendeleo ya nchini yetu.
Kushoto ni Afisa Habari wa Ubalozi Mindi Kasiga akifuatilia kwa karibu anachozungumuza Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara, kulia ni Mhe. Liberata Mulamula nae akifuatilia maelezo ya Mhe. Waziri kwa makini.
Mhe. Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi huo, kutoka kushoto ni Mwambata wa Jeshi Colonel Adolph Mutta, Afisa Paul Mwafongo, Afisa Switebert Mkama, Afisa Agnes Lusinde, Afisa Mindi Kasiga, Mhe. Waziri, Mhe. Balozi aliyesimama nyuma ya Balozi ni Afisa Catherine Kijuu, Mkuu wa Utawala Mama Lily Munanka, Afisa Suleiman Saleh, Afisa Emmanuel Swere Alfred na Afisa Abbas Missana.

No comments: