Tuesday, November 19, 2013

Ana kwa Ana na Astronaut Dr Donald Thomas


Karibu katika mahojiano haya na Dr Donald Thomas.
Mhandisi na mwanaanga wa Marekani
 Katika mahojiano haya, Dr Thomas anaeleza historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi.
Ilimchukua miaka 9 tangu ajaribu kwa mara ya kwanza mpaka achaguliwe, na katika miaka hiyo, alituma maombi mara nne.
Ili kuongeza nafasi yake kufanikiwa akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo.
Lakini aliamini katika atendalo.
Pia ameeleza maandalizi wanayofanya na mafunzo wanayopitia kuanzia wanapochaguliwa mpaka wanapoenda kwenye mission hizo, hisia na uoga wake siku ya kwanza alipanda space shuttle. Amezungumzia safari nzima na shughuli kuanzia wanavyoondoka mpaka wanavyofika angani pamoja na changamoto za kuishi kwenye orbit. Kuanzia kupika mpaka kutumia choo. Na pia, namna alivyopokea taarifa za kulipuka kwa space shuttle Columbia. Shuttle aliyoitumia mara tatu kati ya nne alizokwenda kwenye orbit.
Baada ya miaka 20 aliyofanya kazi kama mwanasayansi wa NASA, na safari nne kwenye Orbit, akastaafu na sasa ni Mkurugenzi wa Willard Hackerman Academy katika chuo kikuu cha Towson hapa Maryland ambapo anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho
Nilipata fursa ya kuhojiana naye mwaka 2011


Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

No comments: