Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa band"
a.k.a FFU watarajiwa kutumbuiza usiku wa jumamosi 23.November 2013
katika ukumbi wa Übersee-Museum mjini Bremen,mchini Ujerumani.
Usikose kuwasikiliza
Wakazi wa jiji la Bremen na miji ya jirani watapata burani ya kung'oa na sululu
kutoka kwa mzimu wa muziki Ngoma Africa band ambayo maarufu sana kwa kuwatia kiwewe washabiki wake kila wapandapo jukwaani.
Onyesho hilo limeandaliwa na makumbusho ya Oversee Museum ya jiji la Bremen kwa kushirikiana na Pan African Organization.
Ngoma
Africa band wataanza kutumbuiza majira ya saa. 4.00 usiku na kabla ya
hapo kutakuwa na maonyesho mbali mbali ya bidhaa za kiafrika,pamoja na
vyakula.
Bendi ya "Ngoma Africa " ambayo inadumu kwa muda wa miaka 20
imetajwa kuwa ndio bendi ya mwanzo ya kiafrika kufanikiwa kudumu katika
medani ya muziki na kujizolea mamilioni ya washabiki katika kila kona
duniani.
Watafiti wa mambo ya muziki wameitaja bendi hiyo kuwa inatumia kila nafasi
waliyo
nayo kuwanasa washabiki wake,na imetajwa mara nyingi kuwa ni bendi bora
na kuchukuwa TUZO za kimataifa, ni bendi ambayo imepachikwa majina
mengi mengi ya utani na kiusanii kama a.k.a "FFU Ughaibuni" ,aka "Watoto wa mbwa" chini ya uongozi wake Kamanda Ras Makunja wa FFF, Mtawala wa
himaya ya " Anunnaki Empire "
No comments:
Post a Comment