Monday, December 9, 2013

Usiku wa Uhuru na hotuba ya Mhe. Makamba Washington DC Metro

Picha kwa hisani ya blog ya Vijimambo
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknologia Mhe. Januari Makamba akiongozana na mkewe Ramona Makamba  wakiwasili ukumbini na kulakiwa na Kaimu Balozi wa Tanzania nchinii Marekani na Mexico Afisa Paul Mwafongo akiwemo Dj Luke wakati walipokuwa wakiingia ukumbini Laurel, Maryland kwenye sherehe ya Uhuru wa Tanzania Bara iliyofanyika Jumamosi Dec 7, 2013 na kuhudhuriwa na umati wa wakazi wa DMV wakiwemo marafiki zao kutoka majimbo ya jirani.
Mhe, January Makamba akiwapa wanaDMV salamu toka Tanzania na kuwaelezea mstakabali mzima wa nchi yetu na kusema miaka 52 kwa binadamu ni mingi lakini kwa nchi bado ni michache aliezezea pia upande wa mawasialiano unavyokuwa kwa kasi na jinsi alivyofarijika kuja kukutana na Watanzania wa DMV na kusema yeye ni muumini mkubwa wa raia pacha kwani anaamini Mtanzania wa Ughaibuni ananafasi kubwa ya kuchangia maendeleo ya nchi yake. Jana Mhe. January Makamba alikutana na WanaDMV Mirage Hall kuanzia saa 11 jioni.
Hii hapa chini ni hotuba aliyoitoa usiku huoKatibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti na Utawala wa Umma Bwn, Georgr Yambesi akielezea mfuko wa pensheni wa PSPF na kuendelea kuelezea faida zake na kwamba sasa mfuko huu umeundwa kutumiwa na hata Watanzania waishio ughaibuni. Leo pia wataongea na Watanzania DMV Mirage Hall Langley Park kuanzia saa 11 kamili.
Dj Luke akiwashukuru watu wote waliofika wakiwemo ujumbe toka Tanzania na Mhe. January Makamba kwa niaba yake biafsi pamoja na waandaaji wengine wa sherehe hii Baraka Daudi na Dj Seif.
Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV akiongea machache na kutoa salamu za Uhuru kwa wanaDMV.
Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchi Marekani Mindi Kasiga akielezea wasifu wa Mhe. January Makamba.

Mshereheshaji Tuma akipendezesha usiku wa Uhuru.

Mgeni rasmi Mhe, January Makamba akishirikiana na Dj Luke kukata keki ya Uhuru.
Meza kuu wakisimama kwa kumkumbuka Nelson Mandela na kwa wimbo wa Taifa.
Mshindi wa tatu wa Miss Tanzania USA Pageant, Faith Kashaa kutoka Alabama akiimba wimbo wa Taifa.
Watanzania wakimshangilia Faith Kashaa baada ya kumaliza kuimba wimbo wa Taifa.

No comments: