Kwa mara ya Kwanza kabisa nchini marekani limefanyka tamasha la Kiswahili katika jiji la Washington,likijumuisha nchi zote za Afrika Mashariki na kati zinazozungumza lugha ya kiswahili.Tamasha hili liliandaliwa ili kuweza kutand=gaza tamaduni za afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na Chakula,Mavazi,Ngoma za Asili,Miziki ya Kizazi Kipya,na mambo mbali mbali ya kiasilia.
Waandaaji wa Tamasha la Kiswahili Washington DC Ndugu Patrick Kajale na Dada Finiana wakijadili jambo na ndugu Safari ambaye ndiye Mtunzi wa kile kitabu Nambari moja Amazon cha Nyayo za Obama.
Ndugu Safari Akionyesha Kitabu cha Obama Patrick Kajale Mwandaaji wa Tamasha la Kiswahili
Afisa Mwandamizi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Munanka akiwa amejumuika pamoja na watanzania waliofika kwenye tamasha hili la kiswahili.
Afisa usalama wa ubalozi wa Tanzania Dr Mkama akiwa na baadhi ya maofisa wa ubalozi.
Maofisa wa ubalozi wakiendelea kula nyamachoma kutoka katika banda la Safari Restaurant DC
Nyama Choma katika banda la Safari Restaurant Washington DC,Safari ni Mgahawa wa Kitanzania uliopo katika jiji la Washington ambapo vyakula vingi vya kinyumbani vinapatikana.
Mishikaki ikiendelea kuchomwa katika banda la Safari Restaurant kwenye Tamasha la Kiswahili
Watu wakiwa mstari kwenye banda la Safari wakijipatia nyama ya motomoto kutoka kwenye grill
Mabanda mbali mbali yakitangaza shughuli zao kwenye Tamasha la kiswahili
Warembo Wakareeeeezz kutoka washington DC na Texas pia walihudhulia Tamasha hili la Kiswahili
Ice Cream au lamba lamba kama zinavyojulikana kwa kiswahili pia zilikuwepo kwa ajili ya watoto na watu wazima
Miss Malaika nae pia hakupitwa akionyesha kuwa "She is Very Confident"
Banda la Wakenya pia lilikuwepo wakitangaza shughuli zao mbali mbali.
Watu mbali mbali wa mataifa yanayozungumza kiswahili wakiwa wametulia kivulini wakipata vinywaji baridi na kubadilishana mawazo.
Wacheza Tamaduni hawa walihalikwa maalumu kutoka nchi isiyozungumza kiswahili ya Ivory Coast.
Miss Temeke- CEO wa Kwetu Fashion Design akiwa katika Meza yake baada ya kumaliza Maonyesho yake ya Mavazi ya Kitanzania.
Walimbwende hawa katika Mavazi ya Kwetu Fashion Design.
Patrick Kajale nae akipita katika Vazi la Kimasai
CEO Wa Kwetu Fashion Miss Temeke Akiwapungia Umati Baada yakumaliza Maonyesho yake ya Mavazi
Juu na chini ni watu mbali mbali wakiendelea kutazama mambo mbali mbali yaliyokuwa yakiendelea.
Kwa Upande wa burudani walikuwepo pia Wasanii Mahili wa kizazi Kipya Wakitanzania na East Afrika kwa ujumla waishio Marekani kama AJ Ubao,Prince Herry,Max na Jumbe Mr TZ
Mwanadada "Senai" Mpiga Gitaa Maarufu kutoka Afrika Mashariki anayeishi Marekani
Mikono Juu..Prince Herry akiwarusha Watazamaji kwa Ufasaha na Style yake ya lay back.
Prince Herry Akifokafoka kwa hisia kali katika kile kibao chake kinachoitwa "Au Sio"
Kijana Max Ambaye watu wengi wanamwita Silent Killer aliwarusha watazamaji vilivyo
Max a.k.a Silent Killer akilitawala Jukwaa kwa ustadi.
Mwanamuziki AJ Ubao kwa nyuma aliwarusha watazamaji na kibao chake cha "Haya ni Maisha Yangu" akishea Jukwaa na Jumbe Mr TZ kijana anayechipukia .
Jumbe Mr Tanzania aliwarusha watazamaji kwa style yake yakipekee huku Mwanamuziki AJ Ubao akimsindikiza kwa nyuma
Jumbe Mr TZ akiwarusha watazamaji akisindikizwa na AJ Ubao
Je waukumbuka Mchezo gani huo?....Mwakani tutaweka pia Bao.
Lamba lamba kwa raha zake.
Waandaaji Wanatoa Shukrani Kwa watu wote waliojitokeza kwani hii ni mara ya kwanza kabisa Tamasha kama hili kufanyika nchini Marekani hivyo tutegemee Mambo mengi Makubwa Mwakani kwani Huu ni Mwanzo.
No comments:
Post a Comment