Wednesday, June 10, 2015

Hatimae Bi Moza afanikisha kumpeleka mtoto wake India kwa matibabu

Bi Moza akiwa  akimshindikiza 
mtoto wake Moh'd Saidi, 
Nchini India kwa matibabu
Bi Moza Moh'd Khamis anapenda tena kutoa shukurani za dhati kwa wale wote waliochangia kwa hali na mali kwa mtoto wake Moh'd Said Moh'd, kwenda kufanyiwa matibabu ya upandikizaji wa figo, nchini India.

Mapema asubuhi ya June 9, Bi Moza aliongea na blog ya swahilivilla ili kutoa taarifa kwa kukamilika safari yake ya kwenda nchini India pamoja na kutaka tumuombe Dua za kumtakia kila la kheri katika safari hiyo.

Moh'd Said Moh'd ameondoka leo Jumanne Juni 9, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuelekea Nchini India kwaajili ya matibabu yake. Napenda kuchukua fursa hii kwa niaba ya Tanzania Bloggers Network (DMV) na waTanzania wote waishio Nchini Marekani, kumtakia kila la kheri Ndugu yetu Moh'd Said Moh'd katika matibabu yake huko Nchini India

M/Mungu amjaalie wepesi katika safari yake na ampe afuweni na mafanikio katika mipangilio yote matibabu yake. Ameen.

No comments: