Tuesday, August 11, 2015

Vodacom Tanzania yapata Mkurugenzi Mtendaji mpya

Dar es Salaam, Tanzania , August 11, 2015
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania Limited leo imemtangaza Mkurugenzi wake mpya Bw.  Ian Ferrao anayechukua nafasi ya Mkurugenzi anayeondoka  Rene Meza ambaye hivi karibinu aliteuliwa kuwa Aisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya  Ooredoo Myanmar kuanzia mapema mwezi ujao.
Ferrao kwa sasa hivi ni Mkurugenzi Mtendai wa Vodacom Lesotho.Ana uzoefu mkubwa wa uongozi katika sekta ya mawasiliano katika nchi mbalimbali za Ulaya na Afrika.Kabla ya kjiunga na Vodacom Lesotho alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu anayesimamia biashara za kampuni ya  Vodacom barani Afrika na alikuwa na hisa katika kampuni ya Africonnect ya nchini Zambia.Ujio wake kuongoza Vodacom Tanzania ni kama vile amerejea nyumbani kwa kuwa wazazi wake waliwahi kuishi nchini tangu mwaka 1952 kabla ya kuhamia nchini Uingereza mwaka 1970.
Akiongelea uteuzi wake alisema “mimi ni mzoefu na nina ujuzi wa kuongoza sekta ya mawasiliano na nina imani sekta hii ni zaidi ya mwasiliano bali imeonyesha mabadiliko makubwa katika kuchangia kuleta mabadiliko kwenye jamii kwa kuboresha maisha ya watu na kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi.Nina imano Vodacom ina uwezo wa kuendelea kuboresha mawasiliano nchini na kuzidi kufanya maisha ya watanzania kuwa murua”
Naye Rene Meza Mkurugenzi aliyeiongoza Vodacom Kuanzia mwaka 2011 alisema kuwa katika kipindi cha uongozi wake Vodacom Imefanya mabo mengi katika kuboresha sekta ya mawasiliano nchini ikiwemo kukua kwa mtandao huo na kuwa na wateja zaidi ya milioni 12 na kuanzishwa kwa huduma ya M-PESA ambayo inatumiwa na wananchi wengi Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi zenye watumiaji wengi kwenye huduma hii kwenye makampuni ya Vodacom Group.

No comments: