Tuesday, September 7, 2010

Natimiza ombi la Prof Matondo

Hapa ndipo nilipokuwa natumika 2001-2003. Still looove it there. Sijui nikirudi watanipokea??????
Kwenye toleo langu la Desemba 19, 2009 kumueleza Mzee Jerome Danford Kassembe (irejee hapa), kakangu Prof Matondo alisema na (hapa nanukuu)"Mzee wa Changamoto - una "clips" zo zote ukiwa mbele ya maikrofoni? Kama unazo, tuwekee hapa bloguni tukusikie ulivyokuwa ukiunguruma."
Nami nilimuahidi kujitahidi kuweka audios zangu za vipindi (ambazo ziko kwenye tapes na katika ubora wa chini) kwenye mfumo utakaoniwezesha kumuwekea hapa naye asikilize, acheke na labda aone tofauti ya kipindi kile na sasa.
Basi nimefanikisha, na japo si katika ubora ambao ninapenda ku-post hapa, lakini naamini zitaweka taswira ya nini tulikuwa tukifanya nyakati hizo.
Sikia mchemko wa "wingi" wa neno chuma kwenye dk ya 14.
Pia katika ku-katakata matangazo na nyimbo nimekuja gundua kuwa neno "msikilizaji" limesikika saana. Kumbuka kilikuwa kipindi kamili nami nimekata na sikuweza kugundua hilo mapema.

Hahahahaaaaaaaaaaaa
FURAHIA

9 comments:

Subi Nukta said...

Mubeeee, afadhali Prof. Matondo aliomba hii na leo umeitimiza ahadi. Saaasa, mi mbona naku-dip sana niko hapa Shell ya OilCom hujibu bwana? Nilitaka kuchangia maoni kuna jamaa alikuwa anavuta sigara ndani ya daladala akashushiwa kipondo cha karne. nhe he! Kipindi kilikuwa murua sana hicho. Kazi nzuri Mube!

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaaaaaa Da Subi.
Nimeshangaa katika yooote hujasikia nilivyochemka (ama umekuwa mstaarabu UKAMEZEA?)
Nawakumbuka saaana Ally Kashushu na Amina Singo
Naikumbuka Times FM na bado naipenda saana
Na sasa hivi ushanifundisha "samsings" nyingi za kuboresha ufikiri na ubunifu kwa hiyo sina shaka siku nitakayorejea "nyuma ya maiki" nitakuwa a little bit wiser kuliko hiyo Aug 23, 2003
Asante mara ya tena kwa kuendelea kutembelea changamotoni

Mija Shija Sayi said...

Mbona sioni ulipochemsha Mzee wa Changamoto? Duuh! wewe ni moto wa kuotea mbali. Hongera sana kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Musee wa changamoto upo juu. yaani duh! hapo kwenye hiyo upweke itabidi uniandikia maana mimi nakushanya vitu kama hivyo. Na mubelwa wala hujachemsha kwa nini Subi akufiche? unapomwona mtu anafanya kosa usisite kumueleza na naamini ungeambiwa. Kazi nzuri sana Mubelwa.

emu-three said...

Heri mimi sijasema,....mkuu upo juu!

Simon Kitururu said...

Poa sana!Bonge la kumbukumbu!

Godwin Habib Meghji said...

Konda naomba msaada kwenye sheli ya BP. Kilikuwa kipindi kuzuri, na kilikuwa na presenter mzuri. Nimesikiliza kwa makini sijapata sehemu uliyochemka. KUMBUKUMBU NZURI

malkiory said...

Mubelwa,ni mtangazaji mahiri sana. Nilijua hivyo siku nilivyomsikiliza live pale East African Radio USA. Sasa tunasubiri Radio Tanzania USA, wewe ukiwa kama mwanzilishi wetu, tupo tayari kukuunga mkono.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nafurahi na kushukuru kwamba umelikumbuka hili. U mtangazaji mzuri sana.

Hapo VOA hawawezi kweli kukupa kibarua japo cha muda tu hasa ukizingatia kwamba Juma Nkamia amekimbia kwenda kuwania ubunge?