Tuesday, April 10, 2012

Let's "Party for a good cause."

Chama cha Wanawake waTanzania waishio Marekani (Tanzanian Women Association-USA) kwa mara nyingine kitaendesha ukusanyaji wa fedha katika harakati zake za kusaidia sehemu / watu ama makundi mbalimbali yenye uhitaji nchini Tanzania.
Chama hiki kinachoundwa na WANAWAKE WANAHARAKATI WA MAENDELEO kinapanga kuendesha ukusanyaji huu wa fedha kwa kushirikiana na Dj Chick and Friends siku ya Jumamosi (Aprili 14) katika ukumbi wa NECTAR LOUNGE uliopo 7926 Georgia Ave.,Silver Spring, MD 20910. Na kama "bango" hilo lionyeshavyo hapo juu, makusanyo yatapelekwa kusaidia kuboresha maisha ya kinamama na watoto nchini Tanzania.
Hii ni awamu nyingine ya harakati za TWA ambao mwaka 2008 waliendesha harambee (rejea post hii) na kufanikiwa kukusanya kiasi kilichofanikisha kununua na kukabidhi madawati 32 yaliyogharimu takriban shilingi Milioni 1.9 (kama ilivyoripotiwa hapa).
Harakati hizi zinaendana na ushauri huu aliotoa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico Mhe. Mwanaidi Maajar kwa wanawake.

Na sasa ni wakati wako wewe mwanaharakati na mwanajamii kuungana na HATAKATI HIZI NJEMA ZA TWA kuwezesha mkakati wa kusaidia kuboresha maisha ya wenye uhitaji.

Vyama ni vingi, JUMUIYA ni nyingi na mahitaji ni mengi, na ni sisi wenyewe tunaohitaji kusimama kidete ili kuboresha mazingira na maisha bora kwa kila mhitaji kwa kujitolea kile tuwezacho katika kufanikisha azma hii. Si lazima kiwe kikubwa, bali tukitoa kwa moyo kitafaa. Kama alivyosema Mother Theresa kuwa "I can do no great things. Only small ones with GREAT LOVE." Nasi tuungane katika kuchangia na kufanikisha kuwaondoa kinamama na watoto katika mazingira haya. Kama TUWA-USA wameweza kusimama katika MALENGO yao kama walivyoeleza HAPA, ni kipi kinachotushinda kuunga mkono harakati hizi?
Licha ya kusaidia kuboresha maisha ya wanawake na watoto nchini na pia kuinua elimu kwa watoto (hasa mabinti) nchini Tanzania, TWA-USA imekuwa ikijitahidi kufanikisha njia za kuwezesha waTanzania walio hapa kujua namna ya kupata elimu bora hapa nchini (BOFYA HAPA)
Unaweza kujua na kujifunza mengi kuhusu TUWA-USA kwa kutembelea tovuti yao HAPA

TUKUTANE NECTAR LOUNGE JUMAMOSI HII.
Let's "Party for a good cause"

No comments: