Inasikitisha saana kuona maisha ya waTanzania tena wasio na hatia yanahatarishwa na hata kupotezwa kwa kile ambacho chaweza kuzuilika. Suala la ajali za barabarani lilishapigiwa kelele na hata kukawepo na "pendekezo" la kukagua na kuthibitisha ubora wa bodi za mabasi kulingana na viwango vilivyopo, lakini tumeendelea kushuhudia ajali ambazo mbali na sababu zinazosababisha ajali hizo, bado kuna uwezekano mkubwa kuwa kuna wanaopoteza maisha na kujeruhiwa vibaya kwa kuwa mabati yanayotumika kutengeneza bodi hizo yana viwango vibovu. Na pia kutojali maisha ya wa-Tanzania kwa KUWALISHA SUMU kutoka viwandani licha ya kero zao kupigiwa kelele saana mpaka Tume ya Mazingira ambayo naamini ilishakifungia kiwanda hivho. Mazingira ya wakazi karibu na kiwanda yapo hatarini na wote wanaotumia maji ya mto Mzinga kwa kuosha magari, kufua, kuoga, kuvua na kwa shughuli nyingine zihusishazo kugusana nayo yamewekwa hatarini na POLI-TRIX zinazoendelea nchini. Sijui wanaohusika wanapewa nini na sijui kama wamechaguliwa na wananchi wanawatumikia kina nani. Labda tusubiri mwakani (kwa kuwa uchaguzi utakuwa unakaribia), tutaanza kusikia wakiyaamsha maana sasa ni siasa tu na si wananchi.
Wednesday, August 27, 2008
Too much POLI-TRIX
Ajali iliyotokes huko Morogoro na kuua watu kadhaa na kujeruhi pia.
Maji yenye kemikali toka kiwandani huko Mbagala, ambayo huingia mto mzinga ambao watu hupata kitoweo toka humo.
Picha zote toka www.haki-hakingowi.blogspot.com
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment