Friday, September 26, 2008

Tufunguke Akili? Come On Latoya

Mshiriki Latoya Lyakurwa (kati) akiwa na ma-afisa wa MultiChoice
Picha kwa hisani ya http://www.issamichuzi.blogspot.com/

Katika mahijiano yake na waandishi wa habari ambayo yamechapishwa katika vyombo mbalimbali na pia video yake inapatikana katika tovuti ya Daily News http://dailynews.habarileo.co.tz/streaming/, mshiriki toka Tanzania katika shindano la tatu la Big Brother Afrika Latoya Lyakurwa amewataka wananchi na waTanzania kufunguka akili zao na kutambua kuwa hii ni "new era" ambapo hatuishi kwenye miti na wala hatuvai majani hivyo inatupasa kukubali kile tunachokiona kwenye Televisheni. Akijibu swali la mwandishi aliyemuuliza anaonaje ama juu ya wale wanaosema kuwa Big Brother haiendani na mila na tamaduni za wa-Tanzania na waAfrika? alisema "... mimi nasema watu wafunguke akili. Utandawazi, yani ni kwamba (kicheko) nilikuwa nataka tu niwaambie kwamba yaani wafunguke mawazo yao yaani kwamba sasa hivi hii ni new era, yaani tuko katika maisha mapya hatuishi tena kwenye miti, hatuvai majani, kwa hiyo hata kuangalia vitu kama hivyo kwenye Tv inabidi tu-accept, kwa hiyo it's a new era, kwa hiyo tufungue akili zetu na tujue kwamba huu ni utandawazi"

Vinavyonisumbua hapa ni vitu hivi vichache ambavyo ni
1: Latoya hakujibu swali la kama anakubaliana nao ama la katika suala la kuendana na mfumo wa maisha yetu,
2: Nadhani watu wamefunguka akili saana na ndio maana wakaoanisha kile walichokiona ama wanachokiona kinaendelea kwenye mchezo huo na maisha halisi ya jamii yetu.
3: Utandawazi na "New Era" vina mengi yenye upana wake lakini si kweli kuwa kila kionekanacho kwenye Tv kikubaliwe kwa kuwa tu ni "new era" ndani ya utandawazi
4: Kwa yeye kuona sasa kuwa hatuishi kwenye miti na kula majani hivyo tunastahili ku-accept kila tuonacho kwenye Tv nadhani ni kipimo cha fikra.
Latoya angeweza kuelezea kwa namna nyingine kwa kueleza mabadiliko ya maisha na michakato ya kutafuta pesa, lakini si kusema kuwa wanaofikiria hivyo hawajafunguka akili na kukubaliana na new era na utandawazi. Ule ni mchezo ambao alikuwa na kila haki ya kushiriki kwa kuwa ulikuwa ni utashi, lakini naamini maadili mengi yanavunjwa na huo ni ukweli ambao kwa waujuao wanaweza kuoanisha hilo na swali ambalo kwa namna alivyolijibu kunaleta maswali mawili. Ama Latoya hajui mila na desturi zinazozungumziwa ama hatambui vema suala la utandawazi na new era aliyoizungumza.
Bado naamini kuwa kuna maadili mengi yanayovunjwa katika mila, desturi na imani za wengi na tunalotakiwa kukubali ni kuwa kuangalia ni utashi kama ushiriki, lakini kueleza ukweli hakumaanishi kuwa hujafunguka kiakili ama kuambatana na "new era".

Ni Changamoto tuuuuuu

1 comment:

Anonymous said...

Ni ushamba tu. Nani kamwambia uchafu wa Big Brother ndio utandawazi?