Thursday, February 24, 2011

Ubora wa jela ni nini na zetu ni namba ngapi?

Najua tuna viwango vya shule na kwa kutumia vigezo kadhaa tunaweza kupewa orodha ya shule kwa ubora. Naweza kuhisi kuwa wanaangalia uwiano wa idadi ya wanaofaulu, wanaochaguliwa kuendelea na masomo, wanavyopata ujuzi kwa wale wasomeao fani mbalimbali na hata mazingira na maisha baada ya chuo ama shule. Najua hata vyuo kama vya habari ama sheria ama uinjinia huwa vinaheshimika kwa kuangalia ni nyota wangapi wanaofanya kazi zao vyema ambao wamepitia katika vyuo ama taasisi hizo.
Sina hakika na Magereza. Ila nijualo ni kuwa sijawahi soma ushuhuda wa mfungwa yeyote ambaye amefanikiwa kutoka jela na kusema maisha ya kule yalikuwa ya kumuendeleza na kumfanya kuwa raia mwema akitoka na kurejea uraiani. Si mnakumbuka mahojiano ya Mhariri wa zamani wa gazeti la Family Mirror Bwn Zephania Musendo aliyofanya hivi karibuni mara baada ya kutoka jela alivyosimulia mateso kuliko mwongozo wa maisha mema ukitoka jela? Alivyoeleza katika mahojiano yake na Mzee wa Sumo Mpoki Bukuku, unaweza kupata picha ya maisha yalivyo na imani ama mtazamo kwamba kinachobadilisha maisha ya mfungwa jela za nyumbani ni MATESO na si mbinu mpya za kujiajiri mara utokako jela. Sehemu ya mahojiano hayo ni hii hapa akisimulia siku mbayo imemuumiza na kumfedhehesha alipokuwa jela, alisema kuna siku upekuzi wa kawaida katika gereza ulikuwa ukifanyika na wafungwa wote walitakiwa kuvua nguo zote na kuchuchumaa.
“Tulitakiwa kuruka kichura, nilipojaribu kuruka na hii hali yangu (ya ugonjwa) nilidondoka chini. Nilitarajia kuwa mtu wa kwanza kunisaidia angekuwa daktari wa jela, ambaye alikuwepo sehemu hiyo. Lakini hakufanya lolote na niliachwa nikigalagala chini.”“Roho iliniuma sana kwa kuwa Bwana Jela pia hakujali bali alisema hakuna taabu na kuwa mimi nilikuwa nazuga tu”.Anasema, alifikiria pale alipokuwa amelala akiwa uchi, kila mtu alikuwa akimwangalia, na kwa kuwa gereza hilo halikuwa na ukuta, basi hata watu wakiwamo wanafamilia wa askari waliweza kumwona.
“Sitasahau siku hiyo kamwe.”
Ni mateso ambayo tumeyasikia na kuyaona kwa mahabusu (kama Wajelajela) wafungwa, na hata watuhumiwa ambao hawajathibitishwa kuwa na hatia ambao wanapigwa na kuteswa badala ya kupewa njia mbadala za kuendesha maisha yao wakitoka jela. Labda sera za jela ni tofauti kulingana na nchi lakini ningetaraji ziwe kama "vyuo vya mafunzo" kama nisikiavyo wakiita ndugu zetu wa Visiwani lakini si mafunzo ya askari kuangalia uwezo wao wa kutesa, bali kuwaonesha waliowekwa huko kuwa huo ni wakati wa kutafakari huku wakipewa "options" za kujifunza yale yanayoweza kuwasaidia watakapokuwa huru na hasa shughuli za kujiajiri maana unajua ajira inaweza kuwa ngumu kupata ukitoka jela.
Ninaangalia baadhi ya nchi zinavyobadili ama kuwawezesha wafungwa wake kubadilika na baada ya hap[o wanakuwa nyota si tu katika familia zao, bali jamii iwazungukayo, nchi na ulimwengu kwa ujumla. Na kwa kuwa mimi ni mpenzi, mfuatiliaji na mshiriki wa ndondi, wacha niwape mifano ya wafungwa waliobadilika na kuwa nyota katika mchezo huo ulimwenguni. Unawakumbuka ama kuwafamu kina Dwight Muhammad Qawi, Ron Lyle, Mike Tyson na hata Bernard Hopkins? Nimzungumzie Bernard Photo Credit: Bernard Hopkins.net
ambaye bado anapigana na hivi karibuni alimpa kipigo cha kwanza mkali Kelly Pavlik. Amenukuliwa akisema kuwa jela haikumbadilisha bali alibadilika mwenyewe lakini hatuwezi kupinga ukweli kuwa katika miaka aliyokaa jela alishiriki mapambano na michuano kadhaa ya ridhaa iliyomfanya awe bingwa mara tatu akiwa huko na kumpa uzoefu na upenzi zaidi wa mchezo huo ambapo alipotoka aliendelea nao na kuwa yota kwa kushikilia ubingwa kwa zaidi ya miaka 10 mfululizo. NiFuture Hall of Famer na sio tu kaleta heshima kwake, bali kwa jamii ya Philladelphia na pia kwa taifa zima. Anapendwa na vijana wengi na wengine wameanza "carrer" yao ya boxing kwa kupenda upiganaji wake na kwa kuwa wamepata nafasi katika gyms atumiazo.

Bwn HARUNA Pembe Mgombela
Labda sipati taarifa hivyo niwaulize walio walio nyumbani, kuna habari za wafungwa kugeuka kuwa mashujaa wa Taifa? Zaidi ya Bwn HARUNA Pembe Mgombela (54) ambaye alihitimu digrii yake gerezani?
Labda tumsake TID aliyeamua kujiita Sauti ya jela atueleze "kwa sauti" juu ya kilichopo huko.
Nisikimbie swali, UBORA WA JELA NI NINI NA ZETU NI NAMBA NGAPI?

Ni mtazamo tuuuuuu.......See you "next ijayo"

3 comments:

Faith S Hilary said...

Inategemea kwa kweli. Sijui kama ni TV imeni-brainwash ama kunifunza kitu kuhusu jela lakini inaonyesha maisha ya jela mbali mbali huko marekani (America's Toughest Jails) - I am sure you are familiar with that. Na kule kuendelea basi ni mtu mwenyewe, ukiwa mkorofi (wapo) basi kuna consequences zake na pia kutokana na nchi mbali mbali...kama mtu angeweza kuwa na hidden camera kwenye jela za Tanzania basi kitakachotoka hapo, not pretty.

Wengine ndio hao wamepata bahati kama huyo bondia hapo, wafungwa pia si wana other activities they can take part to as long as they don't cause any harm? Some don't learn ama sijui inakuwaje, wanatoka halafu wanarudi...hapo sielewi...anyway! Mimi naona kama shule fulani...ukijitahidi basi utasaidiwa kuendelea...lakini si kuna shule tofauti, nchi tofauti na kila mmoja na "controls" zake...As I said I hope I am not brainwashed by what I see on TV in terms of "editing" and also news coverage. Naisha hapo

Life is what you make it, so make it right.

emu-three said...

JELA NII JELA TU! Ndio kuna hata waandishi wengine walitunga vitabu vyao wakiwa jela, lakini asikudanganye mtu kuwa jela ni sehemu inayoweza kumbadili mtu. Na ubora wake labda ni kwa kula vizuri, kuangalia runinga, lakini yale mateso, uonevu, uvunjaji wa haki za binadamu nk, kote ni vile vile.
Kwasababu mle mnachanganywa na watu vichwa maji, ambao kiukweli ni `wabaya' na huko watatumia ubaya wao kuwaharibu wengine!
Kitu kama jela, kilitakiwa kiwe kweli chuo cha mafunzo, humo kuwa na wataalamu wa akili, wataalamu wa kila nyanja, ili huyo mtu aliyeharibikiwa `kiakili'akitoka awe amebadilika. Mtu kuwa mwizi, muuaji nk, ni kuharibikiwa kiakili!
Wengi tunaowajua waliotoka jela, wameishia kuugua magonjwa kama sio TB, NI UKIMWI, UKURUTU NK.
Watu wababe ndio watakaofanikiwa kwasababu watautumia ubabe wao kujilinda, na kama kuna nafasi kama hizo za boksi, miereka, haaa, basi huyo atakuwa kawini. Lakini wanyonge, na ambao utakuta walifungwa kibahati mbaya, kama sio presha, atatoka akiwa na magonjwa yasiyotibika!
Watu wa haki za binadamu, wajitahidi sana kulitizama hili na kushinikiza kuwa humo jela, kubadilishwe utaratibu...ndio mtu huyo ni mkosaji , lakini `utu' wake, na ili abadilike inatakiwa juhudi za kibinadamu!La sivyo `unamtia adabu' kama wasemavyo,kwa kumuingizia usugu na ukatili akitoka, kama sio kumpa magonjwa ya kujifia au kuambukiza wenzake!

Anonymous said...

Siku zote mtoto akikosa na akikubali kama amekosa na kuwa mpole kutumikia adhabu yake basi huyo ni mtoto mzuri,na yule ambaye ana kataa kama ajakosa na wakati amekosa na adhabu yake anatumikia kwa shingo upande,basi huyo sio kijana mzuri,Kwa wafungwa ni hali hiyo hiyo unapokosa na kufungwa unatakiwa kujifunza mengi na swali la msingi umefikaje pale na umeweza jifunza nini ili wengine wasirudie matatizo hayo.Kwa system ya magereza ya Tanzania ni uzembe au watu(viongozi)kutothamini wananchi wao,maana kama wagekuwa wana jali mengi yasingetokea,kuna shida ya maji kila greza la tanzania,urasimu wa kuwaona wafungwa kama wewe sio ndugu,yako mengi ila muhimu tunapaswa kuwadilisha utaratibu mzima wa uendesha ya magereza yatu.
Ubora wa jela utajulikana kwa kutoa wafungwa wasiorudia kosa wengi kwa miaka mingi.Pamoja tunaweza kuelimisha wengine.