Tuesday, December 9, 2008

SHEREHE ZA MIAKA 47 YA UHURU WETU

Ni kweli. Namna nionavyo tatizo ndilo tatizo.

Kama shule hii ina miaka zaidi ya 47, basi ni lazima ilikuwa na hali nzuri kabla ya uhuru kuliko sasa

Na naamini hii imejengwa ndani ya miaka 47 ya uhuru, sasa sijui tuseme hatuthamini shule zetu ukilinganisha na waliotutawala. Mmmmmhhhhh!!!!!!!!!!
Picha zote toka kwa Dr Faustine

Naamini waTanzania tunastahili kusherehekea miaka 47 ya Uhuru lakini bado naamini namna nionavyo sherehe hizi zikiadhimishwa yaweza kuwa tatizo.
KWANZA nategemea kutakuwa na GWARIDE kuuubwa ambalo najua linawachukua ma-askari muda wa kutosha kuliandaa. Na amini usiamini linagharimu katika maandalizi yake. Lakini gwaride hili ni la nini, la nani, kwa nani ili kiwe nini? Namaanisha yamfaa nini Rais kukagua "maigizo" ya ukakamavu ilhali hali ya mwananchi wa Nanjilinji na Rubafu ni mbaya? Ni kwanini tutumie gharama zote hizo kuandaa gwaride ambalo mwananchi wa kule Natukuvaja sio tu hataliona, lakini hata kulisikia hatalisikia maana wengine hata redio hawana na wenye nazo hawana betri kutokana na uchumi mgumu na mgawanyo m'baya wa kipato unaoendelea kukua nchini mwetu. Halafu tukimaliza kuangalia gwaride tunaanza kufikiria itatuchukua muda gani kurejesha nyazi za uwanjani mwetu. Dah!!!
PILI sitashangaa hata yule Mbunge wangu wa nanii ambao sote twatokea pembezoni mwa nchi akijumuika kwenye yale yaitwayo MAADHIMISHO YA KITAIFA (na nahisi anasafiri kwa gharama za serikali) na kuwatelekeza wananchi wake ambao hali zao kwa ujumla si nzuri hata kidogo. Kama kuna anayedhani huu ni mtazamo wangu na afanye tathmini kwa kupiga kura za maoni kujua ni wangapi wanapenda sherehe za Uhuru ziadhimishwe kama ziadhimishwavyo sasa. Naweza kuwa na Uhakika kuwa kutatakiwa mabadiliko.
TATU labda niache kujiuliza mwenyewe na niweke hapa ili wenye uerevu (ama muonao tatizo hili kwa namna nyingine mniambie). Kuna umuhimu gani wa kualika viongozi, kuwagharamia chochote muwagharamiacho (kuanzia usumbufu kwa wananchi kwenye masuala ya ulinzi wa viongozi hao mpaka gharama za nchi zao kama si sisi tunaozilipa) kisha wakaja pale kusikia ni asilimia ngapi ya wafungwa wataachiwa huru na "politrix" nyingine? Huu mfumo ama mtindo wa kusherehekea Uhuru namna hii ni asili yetu? Ama tumepata kwa nani na kwanini wao wanafanya hivyo? Hivi ni lazima tuendeleze haya? Kwani yana manufaa gani kwa wananchi wetu hasa wa kima cha chini?
NNE niseme kama ningepata nafasi ya kutoa maoni ya namna halisi ya kutekeleza haya, basi ningeona kuwa ni wakati muafaka wa kuangalia mipango ya mwaka iliyowekwa mwaka jana, kuona ni mingapi imetekelezwa na mingapi imeshindwa kufanikisha nia na malengo ya kuwepo kwake. Iwe kama Birthdays (hata hivyo si ni birthday ya nchi huru?) ambapo mtu anaweka "wishes" zake na mwisho wa mwaka anaangalia kama zimetimia. Kwanini huu usiwe wakati wa kutathmini mwaka kiutendaji? Kwanini siku kama ya leo isionekana kutafuta UHURU WA MAISHA YA WATANZANIA WA CHINI? Ina maana gani kuwa na kile kiitwacho uhuru wakati watu vijijini hawapati huduma za afya, hawana habari ya nini chaendelea nchini mwao, hawana maji safi, elimu yao ni duni na haki ndani ya maisha ni yao ni ya kununua (rushwa)? Najua wapo watakaotaka kulinganisha maisha ya sasa na miaka 47 iliyopita na kusema kuwa tumeendelea kwa kuwa na maghorofa mengi, wasomi wengi, wataalamu wengi, barabara pana, uzalishaji mwingi na hata teknolojia iliyokuwa, lakini kwa hakika nyuma ya kile kionekanacho kama maendeleo kuna mapungufu makubwa. Angalia sasa miaka yetu 47 ya Uhuru ilivyotuunganisha na "maendeleo" ya jumla ya ulimwengu, more Degrees but less common sense; more knowledge but less judgment. More experts but more problems; more medicine but less wellness. We’ve learned how to make living, but not a life; we’ve added years to life not life to years. Fancier houses but broken homes.

Kwa hakika huu ni mtazamo wangu wa sherehe hizi za Uhuru. Naamini tunastahili kubadili namna ya kuzisherehekea na kuzifanya kuwa za kijamii zaidi. Zikiwahusisha wenye kuhitaji UHURU wa maisha na kuweza kusherehekea zaidi kile ambacho mababu zetu walipigania na kuomba kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo. Kutathmini na kutatua matatizo zaidi ya kuendeleza kwa kugharamia mabo yasiyo na manufaa kwa TAIFA ZIMA.
Nina hakika kuwa NAMNA NIONAVYO HILI TATIZO YAWEZA KUWA TATIZO.



5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Sio tatizo Ni TATIZO! kwani ni kweli kabisa inaonekana wakoloni wameondoka lakini bado kuna wakoloni ambao ni waTanzania wenyewe wanafanya vitu ambavyo si sahihi kwa waTanzania wenzao bila aibu na bila huruma. Hakuna haja ya kupoteza gharama zote hizo wakati watu vijijini wanahitaji.

Ni kweli kabisa hii sherehe ni kwa ajili ya nani. Kama si ya wote walio huru? lakini kwa sasa inaonekana ni ya viongozi ambao hawafikiri UHURU NI NINI?

Unknown said...

Mimi naona kwamba haina haja ya kusherehekea uhuru.
Hivi ni uhuru gani tunaosherehekea ilhali mpaka leo hatujaweza, kujitegemea?
Baada ya kupata uhuru mwalimu alianzisha siasa ya ujamaa na kujitegemea, sasa je ina maana miaka yoooote hiyo tumeshindwa kujitegemea?
Siamini kwamba nchi inaweza kujitawala wakati bado inategemea misaada toka kwa hao hao aliowadai uhuru.
Ni lazima watakutawala tu.
tatizo letu kubwa katika nchi hii hatuna viongozi wabunifu, hasa viongozi tulio nao sasa.
Naomba niwe mkweli kwamba Raisi wetu hana wasaidizi wabunifu, kila jambo linasubiri mpaka yeye aseme.

Kuna wakati namuangalai Muheshimiwa Rais wetu kisha namuonea huruma.
Akifanya ziara mikoani, utashangazwa na taarifa za viongozi wetu.

Hotuba zimejaa takwimu za ku copy na ku pest.
Kinachozungumzwa ni tofauti kabisa na hali halisi, Muheshimiwa Raisi anadanganywa hivi hivi, WIZI MTUPU!!!
Hatuwezi kusheherekea uhuru wakati viongozi wameshindwa kutimiza yale waliyoyaahaidi tangu tulipopata huo uhuru.
Miaka 47 ya uhuru! lakini mpaka leo, hakuna huduma bora za afya, maji safi ni ndoto, elimu imejaa migogoro kila kukicha,
Wao wamesomeshwa bure, halafu wanataka sisi tulipie Elimu. WIZI MTUPU!
Viongozi wetu wamekuwa wabinafsi wa kujilimbikizia mali, kiasi cha kuwa na ukwasi wa kutisha, halafu wakiulizwa wanasema eti ni VIJISENTI!
Naona niishie hapa, niwapishe wengine nao wachangie.

Christian Bwaya said...

Nadhani umefika wakati huu unaoitwa "uhuru" utizamwe kwa uangalifu. Sababu ni kwamba maadhimisho haya yanakuwa kama mchezo wa kuigiza.

Nikupe mkono kwa changamoto nzuri uliyotupa. Sikuwa imefikiri kabla: Hivi mgwaride wote ule ni wa lazima? Watu wala miayo, mwawapichezeaw gwaride?

Kuna haja ya kusherehekea uhuru (kama kweli tunao) kwa njia nyingine.

MARKUS MPANGALA said...

Dada Yasinya!! wakoloni hawajaondoka hilo naomba ufanye uatifi tena na kama mimi mdogo wako naongopa nisute dadangu{ningeweza kusema hilo lakini turudi katika hoja ya uhuru} kimsingi uhuru tunastahili lakini kinachokera pia kwamba jamaa ughaibuni wanasema tunasherekea tangu watuhurumie na kutuachia nchi zetu[wali waliziacha lini na sa ngapi?} Kwa hawa watawala wetu!! huwa napata wazimu wakati mwingine! ndiyo maana niliwahi kuandika makala moja kuhusu kupaganyika kwa CCM{chai, chapati, maharage}, kwamba ukishajenga kundi katika chama siyo wote watakuunga mkono, nikasema nimesoma sayansi ya siasa na naendelea kusoma hiyo, nikasmea ni ujinga kutumia muda wako kama kiongozi kujingea kisiasa badala ya kujenga msingi wa maisha ya wananchi. hapo ndipo tunapokosea sisi watanzania{na pengine nimejaribu kuandika makala katika gazeti la RAI ambayo itatoka alhamisi hii sehemu ya kwanza} kwamba makosa yaliyoanza toka kale iwe kwa kukusudia, waliwaridhisha watawala wetu ujuha{kwa bahati mbaya hawakujua} kasumba hzii ni kwamba ukiangalia mfumo wetu wa uongozi katiba inasema Rais anaweza kuamua lolote bila kuulizwa na mtu{what?} sasa hapo utakuta maamuzi ambayo yanashangaza sana na kwa mfano kosa ambalo linafanyika kwa utawala wa awamu ya nne hii ni kukosa kipaumbele. Rais wetu amejikuta natakiwa kushughulikia ujuha uliofanywa na akina Mwinyi, kwani kuacha sera za ujamaa kwa kisngizo hazitekelezeki illikuwa kosa kwasabau hakuwa na msingi wa kujiingiza katika ubepari. Pia hakuna ubepari asilimi 100 bila ujamaa? mafno hii sera ya George Bush ya 'ukwamuajiwa sasi za kibenki' hii ni sera za ujamaa. Sasa ujinga uliofanyika ni kudanganywa kidogo na hawa wakoloni, lakini sisi wenyewe tukakubali ujinga{ hapa nakumbuka maneno ya mwanahip hop wa bongo JOH MAKINI;"wanawafanya ujinga, kudanganya toka awali nasi tunakubali ujinga, hii inachangiwa na masaka wanaobisha kama jambo la msingi ni ku-keep it real}. sasa hatuna msingi, hatuna sera, hatuna mweleko= tumepotea njia. Pamoja na kwamba huwa naamini ndiyo tunaingia katika ubepari wa kweli tokana na huu ufisadi lakini inaonyesha makosa ya wazi akama alivyosema Nyerere kwamba MKIFUTA AZIMO LA ARUSHA MTAPATA SHIDA SANA HUKO MBELE. lakini kasema hilo siyo agizo la mungu kama wanaona halifai waache. sasa pale tulioonda msingi tukarukia mambo kila kitu harijojo sasa. China wanajua kwamba msingi wao ni ukomusti kwahiyo wanapoingia katika ubepari wa mlango wa nyuma wanajaribu kuyaacha yale ambayo yanakwamsha mambo katika ukomunisti wao, kwahiyo wanajaribu kuondoa vikwazo katika ukomunisti na kuingia kidogo ubepari. Tunarudi palepale kwamba hakuna ubepari bila jumaa na kinyume chake.siwezi kusema china ni mabepari kwa sasa au ni wakomunisti ingawa wanaendeshwa na sheria nyingi za kikomunisti.
kwetu uhuru bado hauna maelezo, hakuna utashi maana uhuru ni wa viongozi waliovalia suti huku wakinukia pafyumu za Paris na viatu vya DIOR ufaransa. nilikuwa nazungukazunguka tu leo kuna watu hamasa zao. hakika nakwambia kuna watu hawana hata habari za hii siku ila sisi tunaojifanya tumebukua na kuwaibia wananchi ndiyo wenye kushupalia. swali JE UHURU NI NINI?

Mzee wa Changamoto said...

Asante wanaCHANGAMOTO WENZANGU. Yaani nchi yangy naipenda ila kuna wakati yanisikitisha. Hasa pale alipogusia Bwn Shabani kuwa twahitaji maendeleo kwa kufuata sera za Mabepari ambao kila sekunde wanawaza kuitawala duinia. Nasi twaamini watatufanya tuwe na nguvu kama wao, na wao wamtawale nani? Kaka Bwana na Kaka Markus sina la kuongeza. Maelezo mema saana na kama kawaida Dada Yasinta nashukuru kwa kutupambazua. Najua kuna wanaoona tatizo la namna tuonavyo. Lakini si kazi yetu kuwalazimisha kuona tuonavyo maana NAMNA TUONAVYO TATIZO NDILO TATIZO