Wednesday, December 10, 2008

SI NILISEMA!!????

Tabasamu la rais ni hili

Fikra za mwenzangu ni hizi
Ulinzi kwa waheshimiwa ni huu
Kwa wenzangu uhakika wa usalama ni huu.
Picha kwa hisani ya Dr Faustine
Niliandika jana na ni kwa kuwa sikutabiri. Nilikuwa najua "maigizo" ya uhuru wetu. Na naomba nieleweke kuwa naupenda na kuuheshimu ila nachukizwa na namna watu wanavyoshindwa kuwa wakweli katika haya. Ni kweli kiongozi wa nchi anaweza kutabasamu namna aonekanavyo rais wetu kama angekuwa akijua hali halisi ya huko vijijini? Ni kweli anaweza kuwa na usalama wa namna ionekanavyo wakati walio vijijini wanahatarishiwa maisha yao na kila aina ya hatari kuanzaia nyumba zenyewe mpaka mazingira ya maisha yao? Sitegemei rais aende kuwapelekea maji ama kuwajengea nyumba ama kukarabati shule zao. Lakini sera nzuri zenye uwazi na kutambua walivyo zingehimiza utendaji wa kuwakomboa hao waishio huko.
Naomba kusindikiza SHEREHE ZA UHURU na kibao chao Morgan Heritage kisemacho A Man Is Still A Man. Wasikilize wakiwaeleza walimwengu kuwa "a man is still a man, whether him wear jacket and tie or walk a bare foot, the only different is, whether him good or rebel. A man is still a man whether him rich or poor, black or white for sure, the only difference is, whether him good or rebel" wanaendelea kwa kusema "Lots of different people in the streets wiping car glass windows. This is what they do day to day just to get a little food to eat. Then you have others wearing suit and tie, work a good nine-to-five. And they take it for granted that they're living a better life"
Hapa ujumbe wa kusindikiza siku hii ni kwamba kuna haja ya kujali watu wa uwezo wa aina zote bila kujali aina ya kazi watumiayo kupata "mkate wao wa kila siku"
Bofya player uwasikilize Morgan Heritage

7 comments:

Unknown said...

Leo umenikumbusha kibao cha Hayati Lucky Dube cha Political Games.
Hebu someni Mashairi haya hapa chini, muone jinsi mwanamuziki huyu alivyowachambua viongozi wa Afrika.

How do you feel when you lie?
Straight faced while people cry
How do feel when you promise something
That you know you’ll never do
Giving false hope to the people
Giving false hope to the underprivileged

Do you really sleep at night?
When you know you’re living a lie
To you it is just a job
To the people it hurts to the bone

What do you say to the orphans?
If the woman and men you sent to war.
What do you say to the widows?
Of the men you sent to war
Telling them it is good for the country
When you know it’s good for your ego
What a shame.
Do you really sleep at night?
When you know you’re living a lie
You talking tough, you talking sincerely

Giving false hope to the infected
Giving false hope to the affected.
To you it is just a job
To the people it hurts to the bone.

Simon Kitururu said...

Kazi ipo!

Mzee wa Changamoto said...

Ndio Kaka Shabani. Kwa kuwa umeweka mashairi, basi natumai nitaweza kuutumia huu wimbo kwenye section ya Them, I and Them katika kuzungumzia waliyosema hawa waheshimiwa wanamuziki kwa hadhira yao (ambayo kwa Lucky ilikuwa ni viongozi). Kaka Simon, kazi ipo tena kubwa. Tupo pamoja na tuone namna mambo yanavyokwenda kutakuwa na nini MAWAZONI mwa mtanzania wa kawaida
Blessings

MARKUS MPANGALA said...

Mmimi hoi kabisa naangalia tu kama yule jamaa wa kitabu cha The Beautiful Once are not yet born kuna jamaa anajitambulisha kwa majina ya Walking corps, walking stick, the seer,na the watcher. mmm UHURU na KAZI au UHURU na UWONGO????
imenishinda hii mada nipo hoi kwaheri kwa leo

Fadhy Mtanga said...

Ni kweli kweli kweli kweli kweli tupu. Kwenye ahadi 10 za mwana TANU, chama baba wa walichonacho sasa, ahadi moja ilisema, "nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko."
Wacha tuseme ukweli!
Hapo ndipo Lucky Dube akatuuliza, "do u wanna be, a well fed slave or the hungry free man?"
Hakuna cha kutufanya tutabasamu.

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli hii sio haki kabisa inakuwa kama hawa viongozi hawana roho kabisa. Nauimia sana.

Anonymous said...

Napenda kukubali kazi yako kaka kwa kutetea haki ya mtz. Ni kweli yametokea na yanasikitisha sana kwa kipindi hiki. pesa kubwa imetumika kutengeneza nguo za watoto wa alaiki ktk sherehe hizo wakati waalimu wanachuo wastaafu wakulima na watu wote wanadai pesa zakujikimu. its not fair ila kwa mtazamo wangu naona ya kuwa twapalilia long term causes za vita. Ni hayo tu but keep it up Bro

Alindwa Bandio