Tuesday, December 23, 2008

Thanks. You are my all HEROS

Mwaka unamalizika (kwa mujibu wa kalenda itumikayo) na katika mwaka huu tumeona meengi saana mchanganyiko. Tumeona ya kusikitisha na kufurahisha. Tumeona kukosoana na kusifiana katika jamii. Lakini mbali na kukua kwa upashanaji wa habari katika nyanja na njia mbalimbali na pia kuzaliwa kwa "zana" za habari kama hii blog, tumeona pia kuelezwa na kuwekwa wazi kwa matatizo na pia wengi wakijitokeza kuyatatua. Hawa ni watu binafsi, mashirika na makampuni (kama ya simu) ambayo yameweza kugusa saana wale wenye uhitaji kwa namna ambayo binafsi imenigusa.
Blog ya CHANGAMOTO YETU inapenda kutoa shukrani kwa wote ambao kwa namna moja ama nyingine wamejitolea kuwasaidia hawa wenye uhitaji wa hali ya juu, na wale waliowezesha kutambulika kwa uhitaji huo. Pia shukrani binafsi kwa wale wanaowezesha kuwepo na kujengeka kwa blog hii na nyingine mbalimbali ambazo kwa namna moja ama nyingine zimeweza kuelimisha ama kuonesha juu ya uhitaji huu. Naweza kuwaeleza kuwa japo hamdhani mfanyacho ni kikubwa, lakini chaweka tabasamu na baraka maishani mwetu.
Naomba (na narejea tena kuwa naomba) wewe usomaye (ambaye tayari kwa muda wako unawezesha mafanikio ya blog hii na nyingine) utambue kuwa ni SHUJAA nikiamini usomapo haya utaondoka na mtazamo chanya wa kuikomboa jamii. Hilo ndilo lengo la Blog hii (na naamini na nyingine nyingi) KUIELIMISHA, KUIBURUDISHA na KUIKOMBOA JAMII YETU TOKA KATIKA UTUMWA WA KIAKILI ULIHARIBIA JAMII YETU.
Naomba nisindikize shukrani zangu naye Lucky Dube aliyewaeleza HEROES mbalimbali kwenye wimbo wake alioupa jina hilohilo, Heroes.
Blessings

7 comments:

Unknown said...

MZEE WA CHANGAMOTO, KWANZA NINGEPENDA KUCHUKUWA NAFASI HII KUKUPONGEZA KWA CHANGAMOTO ZAKO NYINGI UNAZOENDELEA KUTUPA KILA SIKU.
KWA KUWA SINA BUDI KUFUATA KALENDA ILIYOTUNGWA NA AKINA BULICHEKA, KAMA ANAVYOITA KAKA KITURURU, NAOMBA NIKIRI KUWA MWAKA HUU ULIKUWA NA CHANGAMOTO NYINGI.
TUMESHUHUDIA UJIO WA BLOG NYINGI ZIKIJA NA CHANGAMOTO TOFAUTI TOFAUTI ZINAZOGUSA MAISHA HALISI YA MWANAADAMU WA LEO.
SINA SHAKA MWAKA UNAOKUJA KAMA TUKIWEZA KUFIKA HUKO TUTASHUHUDIA MABADILIKO MAKUBWA YA KIMAISHA NA KIFIKRA, KWANUI MWANAADAMU WA LEO SI YULE WA ZAMANI ALIYEZOEA KUKARIRISHWA KILA UJINGA ULIOJAA TAKWIMU ZISIZO NA MASHIKO.
NATARAJIA KUONA CHANAGMOTO NYINGI KATIKA BLOG HII.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Kaluse, tunapozungumzia "mapinduzi" katika uelimishaji ndani ya Blog basi lazima tuguse UTAMBUZI NA KUJITAMBUA. Ni kati ya "must read" blogs kwa kila anayependa kujitambua kama ambavyo utahitaji kujielewa ukamkimbilia Bwaya ama kutambua mawazoni ukaenda kwa mwanafalsafa Kitururu na kuyajua maisha mchanganyiko ukamkimbilia Da Yasinta. Ni kama ambavyo utapenda mchanganyiko wa habari kijiweni ukaenda kwa Kamala ama kujumuika na malenga kwa mafundisho na maburudisho ukamkimbilia Ka Fadhy. Kwa sisi wa mbali twakaribia nyumbani kwa kuwatembelea kina Marcus na Mjengwa na wengine wengi ama ambavyo utataka kujua almost kila kitu ukaenda kwa Kaka Michuzi.Blogs ni Nyingi saaana na webs pia na zimeendelea kuwa kiunganishi kikuu kati yetu na wengine wengi. Misaada ninayopata (japo kupevuka kimawazo) kwa kusoma haya ndiyo inifanyayo kuwaona ninyi bloggers wenzangu (Bwaya hapa sisifii naeleza ukweli) kuwa ni maSHUJAA wangu.
Labda mwisho nimshukuru "fundi mitambo wangu" Da Subi kwa namna ambavyo ameni-connect na vi'links mbalimbali vinavyoniwezesha kusisitiza maandiko yangu kwa namna mbalimbali. Jeff Msangi kule Bongo Celebrity na pia kule ninyonyapo taswira za kuweka uzikto kile nielezacho kwa kina Kaka Mroki, Dr Faustine Baraza, Mpoki Bukuku, Michuzi Jr, Haki Ngowi na wengine. Kwa Mwanamaoni wa kwanza humu Mariam Yazawa wa Mumyhery Collection Blog na wana Injili wa Strictly Gospel na Nyimbo za Injili.
Nijumuishe kwa kusema kuwa wale wanikosoao na kuniandikia maoni kwa namna moja ama nyingine wananipa mwanga wa nini natakiwa kuboresha, kuacha na ama kuendeleza na kwa wale wote wasomao na kukosa muda wa maoni nanyi nasema asanteni. Kwenu nyote msomao sasa, THANX. YOU'RE ALL MY HEROES.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Sitasema sana kwani yote yameshasemwa. nakutakia kila la heri wewe pia na nasuburi Changamoto zaidi 2009.

Subi Nukta said...

Mahali ni pazuri, Ndugu wanapokaa,
Wakipatana vyema na wakipendana.

Kama umande mzuri, Unyeshavyo shamba,
Hivyo na Mungu wetu, abariki ndugu.

Upendano hujenga, boma zuri kwao,
Wakae na amani...

Na ulimwengu wote, wapita nuruni,
Halafu kundi moja,....

Mwaka 2009 uwe wa mafanikio na barka tele!

Simon Kitururu said...

Asante sana wewe pia MZEE wa changamoto!Na ni kweli ,Bila changamoto hata chamoto kinapoa!

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto. Ulimwengu wa blogu kwangu ni mpya na sina zaidi ya wiki mbili tangu "niigundue" blogu yako lakini tayari nimekuwa mdau mkereketwa. Mtazamo wako ni chanya, fikra zako ni pevu na ye yote anayetembelea blogu yako ni lazima ataondoka na kitu cha kumfanya afikiri (kama anataka). Kauli mbiu yenyewe tu - the way you see the problem is the problem - inatosha kabisa kutekenya fikra dadisi na kumfanya mtu asaili upya baadhi ya mitazamo yake. Uendelee kuhekimika ili uendeleze libeneke mwaka ujao. Sikukuu njema ya Krisimasi na mwaka mpya (2009) wenye heri!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Shabani, Da Yasinta, Da Subi, Kaka Simon na Mwl Masangu. Hakuna zaidi ya sante kwenu. Nynyi ni kati ya wale ambao mwanifanya niendelee "kukua' katika utendaji wa kazi. Nimewataja wengine na kuna ambao sitaweza kuwakumbuka (si kwamba nimewasahau) lakini nashukuruni kwa muda wenu wa kuacha maoni hapa, nawapenda, nawaheshimu na nawaombea saaana.
Baraka kwenu