Friday, December 5, 2008

Them, I & Them: MORGAN HERITAGE ......... Nothing To Smile About

Nikiwa na Mr Mojo wa Morgan Heritage
Pengine tunapoelekea kwenye kuadhimisha miaka mingi ya uhuru na pia kukamilisha mwaka wa tatu wa awamu ya nne, ni vema tukajikumbusha juu ya yale ambayo pengine hayaoneshwi kwa uhakika na matokeo yake kuficha ukweli wa maisha halisi ya mtanzania. Sote twajua matumaini waliyokuwa nayo waTanzania mara walipopata Uhuru na twajua matumaini tuliyokuwa nayo na tuliyonayo kwa awamu hii ya nne ya uongozi iliyoingia na Kauli Mbiu ya Maisha Bora kwa kila mtanzania. Twayapenda maisha bora na naamini wengi wa waTanzania wako tayari kusaidia harakati halisi na sahihi za kuyatafuta (sijui kama watu wana moyo huo anymore) lakini bado ukweli unabaki kuwa sehemu kubwa ya Tanzania ambayo haioneshwi kwenye habari ina mambo mengi yanayosikitisha kuliko kutabasamulisha
Kama walivyoimba Morgan Heritage kwenye wimbo wao huu Nothing To Smile About (japo wao walizungumzia zaidi hali ya Jamaica ambayo kwa namna moja ama nyingine yafanana na kwetu), tunasikia jinsi watu wanavyoisifia Tanzania. Kwa Amani, Upendo na "mafanikio ya kuinua maisha ya mtu wa chini" japo kwa wale walio chini wanaona namna mabadiliko yamaanishavyo kuzidi kusubiri bila mafanikio. Ni jambo la kusikitisha sana kama unakutana na mtu anayekusimulia mafanikio haya tena kwa furaha kuu huku sisi tutokao vijijini tukijua hali halisi waishio ndugu zetu ambao tumewatembelea muda si mrefu uliopita. Simaanishi kuwa hakuna maendeleo lakini sidhani hata kama viongozi wetu wanatambua hali halisi wanayokabiliana nayo wakazi wa vijijini ambako hasa ndiko uliko UTI WA MGONGO WA UCHUMI WETU.
Lakini si vijijini tu, hata baadhi ya sehemu za mijini na kwenye maJiji kama Dar na Mwanza ni ya kusikitisha. Tuangalie baadhi ya taswira za karibuni kisha tujiulize kuwa "ukutanapo na mtu, akaanza kusifia takwimu aonazo kwenye tovuti mbalimbali juu ya kile kiitwacho maendeleo ya Tanzani utakuwa na lolote la kutabasamu ukikumbuka haya?" I mean DO YOU SEE ANYTHING TO SMILE ABOUT?
Ni Shule ya Msingi Amani, Ilala, Dar. Wanafunzi 2989, Madarasa 17 na madawati 287. Do you see anything to smile about? Picha toka kwa Issa Michuzi Mtanzania wa leo akikata kiu kwa "maji taka". Do you see anything to smile about? Picha na Rama Msangi
Mwanafunzi. Anakunywa na kuhema nini? Do you see anything to smile about? Picha toka Ipp MediaNi Dar hapa. Do you see anything to smile about? Picha mali ya Mroki

Hebu wasikilize na / ama kuwatazama Morgan Heritage hapa chini walipozungumzia kwao na kusema japo watu wanaisifia na kuitamani Jamaica, wao wanajua kilichopo kwenye mitaa, kwa watoto wanaoganga njaa, hali ya shule ambazo watoto ndiko wanategemea kupata elimu bora na hata hali za kusikitisha kwenye vituo vyao vya Polisi. Kwa Pamoja (Wao na wageni) wanakubaliana kuwa ukizunguka nchini kote na kuona yote, utagundua kuwa there's NOTHING TO SMILE ABOUT.
Wasikilize hapa chini

Ama watazame hapa chini

(intro)
Nuff people come to jamaica and nuh know how we live
Think seh everything nice through we full of vibes and think
Dem say want feelin to dem heart when dem get fi overstand di real thing yeaah

(verse 1)
Mi deh ya a town one day
A par with a white man weh come all the way from no way
And him turn to mi an say
How comes Jamaica full of so much screwface
Same time mi lift mi head to the sky
And a tear drop fall from mi eye
Mi say my youth come we go for a drive
Mek mi sure you why mi cry

(chorus)
Look pon di gully side
Do you see anything fi smile bout
Look at that hungry child di air
Do you see anything fi smile bout
Look at the school weh deh youth dem go fi get dem education
Do you see anything fi smile bout
Look at the conditions of our police stations
Do you see anything fi smile bout


(verse 2)
Same time the bredda say
How can a nation believe in this way
And the next thing him say
How can the government play so many games
Same time mi ?? fall to the ground
Cause dis much war where that comes from
Certain place they are worse dan slum
Youth man come

(chorus)
And take a look pon river town
Do you see anything fi smile bout
Look pon pain land
Do you see anything fi smile bout
Concos mobay and ????
Do you see anything fi smile bout
????????????? all the same
Do you see anything fi smile bout


(intro)
Nuff people come to jamaica and nuh know how we live
Think say everything nice through we full of vibes and think
Dem say want feelin to dem heart when dem get fi overstand di real thing yeaahchorus

(verse 1)
Mi deh ya a town one day
A par with a white man weh come all the way from no way
And him turn to mi answer
How comes jamaica full of so much screwface
Same time mi lift mi head to the sky
And a tear drop fall from mi eye
Mi say my youth come we go poor a dry
Mek mi sure you why mi cry

(chorus)
Take a look pon river town
Do you see anything fi smile bout
Look pon pain land
Do you see anything fi smile bout
Canterberry mobay ???
Do you see anything fi smile bout
Nuff likkle place deh ya inna jamdown today
Weh not no dead fi smile bout

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli hakuna kitu cha kutabasamu, Inaletesha uchungu sana. Sijui nchi yetu inatoka wapi na inakwenda wapi. Kwani viongozi wetu wamesahau kabisa sisi watu wa vijijini kama ulivyosema vijijini ndio uti wa mgongo wa uchumi.

Wanafunzi wanakaa chini na kupata elimu kweli utasoma kitu cha uhakika. Hii sio haki kwani kuna sehemu wengiine wana shule nzuri madawati/ viti vizuri lakini hawataki kwenda shule.

Maji ni lazima kila mtu awe na maji safi na salama. Kwa nini watu wasiwahamasishwe kuchimba visima au kupeleka mabomba vijijini. Jamani leo nimekasirika mpaka sielewi ninachoandika

Anonymous said...

Kweli ndugu yangu. Kuna mengi ya kusikitisha huko kwetu japo hatuyaoni. Nadhani maelezo, picha na muziki vinajitosheleza

Mzee wa Changamoto said...

Mimi wala sina la kusema. Kila nikisikia sifa za Tanzania nashukuru MUNGU huku nikiomba kuwa ziwe za kweli (na najua baadhi ya sehemu zimepiga hatua saaana na twashukuru kwa hilo) ila pia kwa sehemu zilizosahaulika nabaki nikiwaza na kusononeka maana kwa hakika there's NOTHING TO SMILE ABOUT

Fadhy Mtanga said...

Kaka, hakuna cha kutufanya tutabasamu. Walimu wanalazimika kugoma kwani serikali inawayeyusha, kuna cha kutufanya kutabasamu?
Mitihani inavuja, wanafunzi wa vyuo na wanahasimiana na serikali yao. Nani anaweza akatabasamu?
Nimefurahi kufika kijijini kwako baada ya kukukuta kwa da Yasinta. Karibu pia kwangu usome mashairi.

Christian Bwaya said...

Inasikitisha sana kuona namna mambo yanavyokwenda hivi sana. Mwenye mamcho haambiwi tazama. Na wala sidhani kwamba kazi ya kuwazuia watu wasiseme badala ya kutatua matatizo ya msingi inaweza kusaidia. Ni kujidanganya.

Mimi huwa nafikiri hivi ni lini mwafrika ataweza kuweka mbele maslahi ya watu anaowaongoza?

Fadhy Mtanga said...

Kwenye nafsi za ubinafsi hakuna anaejali maslahi ya anaowaongoza. Kaka Bwaya, viongozi wa sasa wanajali maslahi yao na ya wale waliowapa pesa za kampeni. Unadhani tunao ujasiri wa kutabasamu? Na hata kama tungekuwa nao, sababu hatuna.
Huwa najiuliza mara lukuki, kuna watu (wenye kushika mipini) wanaoyafeel matatizo ya jamii? Kabla mtu hajanijibu tayari nakuwa nimejijibu, hakuna. Hapo tutatabasamu vipi? Hatuna sababu.
Hatutakuwa na sababu hadi pale sababu itakapojidhihirisha.
Lakini tunayoimani kuwa siku moja wema utashinda uovu.
Ni hayo tu kaka zangu.

Unknown said...

Do we have anything to smile about? I do..We as human beings fail to recognize the little blessings and keep looking for what we want to see. Waking up in good health in itself is a blessing(something to smile about) even if you have no job and no idea if you will have the next meal or not. The bible says, Matthew 6:25-34
"Therefore I tell you, do not worry about your life, what you will eat or drink; or about your body, what you will wear. Is not life more important than food, and the body more important than clothes? Look at the birds of the air; they do not sow or reap or store away in barns, and yet your heavenly Father feeds them......

We dont have as much 'wants' and not even the neccessary 'needs' but as much as concentrate in amassing wealth we we always be searching but if we learn to be content with the little we have, then we will know when we are blessed and in abundance..