Monday, December 29, 2008

Umemshukuru ama kumuombea adui yako??

Ndioooo!!!
Nauliza kama umeshamshukuru adui yako. Lakini kwanza adui yako ni nani?
Na anakufanya wewe uweje? Jasiri? Ujitegemee? Utambue upande wa pili wa binadamu wengine? Uwe na maamuzi ya haraka na yenye kukulinda wewe? Kufikiria namna ya kutoanguka aamuapo kufanya jambo kwako? Ama afanyaye lipi?
Lakini yote haya si yana umuhimu kwako? Yaani ukishajiandaa hivyo halafu akafa leo, akianza kutokea mwingine hudhani kuwa utaweza kumkabili kabla hajafikia kiwago cha uharibifu? Wewe waonaje?
Na kumbuka si lazima uone nionavyo mimi maana NAMNA UONAVYO TATIZO NDILO TATIZO.
Lakini niliandika kwa Kaka Bwaya kuwa kila mtu ana nafasi na wakati mwimngine wahitaji mawazo ya kweli ya wale wakuchukiao kuweza kujengeka zaidi. Bwaya tena alishauliza juu ya akusifiaye na akukosoaye na pale pia tukasema kuwa kusifiwa na kukosolewa vyote vyaweza kukujenga ama kukubomoa kulingana na mtazamo wako.
Rudisha fikra nyuma kisha utazame ni wangapi walisema huwezi kufanya hiki na ukasema unaweza na kwa kuwadhihirishia kuwa unaweza ukajifunza meeengi sana ambayo pengine usingeyajua kama si kutumia njia uliyotumia kutaka kuwaonesha kuwa uko sahihi? Ni wangapi wametambua msimamo wako na ushujaa wako kwa kuwa tu umeweza kukabiliana na vikwazo fulani? Unajua kuwa ushujaa wa kweli hutokana na vikwazo?
Na unadhani vikwazo huletwa na nani? Si adui?
Basi adui ana nafasi gani katika maisha yako? Pengine vikwazo ndiyo "shehena" kubwa ya furaha unayoweza kuwa nayo mara uvipitapo.
Hebu sikiliza SHUHUDA mbalimbali zitolewazo na watu. Jinsi ulivyopita maisha magumu zaidi, ndivyo ushuhuda wako unavyokuwa na nguvu zaidi na ndivyo unavyowagusa wengi na kubadili mitazamo ya wengi wenye shida kama wewe. Nelson Mandela alinukuliwa akisema "The greatest glory in living lies not in never falling, but in rising everytime we fall" Hakuna ubishi katika hili. Lakini pia ni nani anayependa kuanguka? HAKUNA. Anayependa kusimama imara baada ya maanguko? KILA MTU.
Mmmmmhhhh!!
Na maanguko yapo na hatuwezi kuyakwepa, sasa kwanini tusiwe na mtazamo chanya wa kukabiliana na kuyapita haya? Kwanini tukae tukiwaza "kwanini limetokea" badala ya vipi ntajinasua na kuhakikisha sianguki tena? Tutakiwa kukubali changamoto kuwa kama twataka na twajua kuwa kuna maanguko na makwazo, basi lazima tuwe tayari kupita njia hizo kuyashinda na kuibuka washindi. TWATAKA MEDALI BILA KUSHINDANA? Nasio Fontaine alisema "harder the battle, tougher the fight, sweeter the victory" Nadhani yuko sahihi.
Peter Tosh alisema "everyone wants to go to heaven but nobody wants to die" aliposema mengi watu wapendayo lakini bila kutaka ama kujua njia sahihi za kupita kutapata katika wimbo wake Equal Rights.
SIWAPENDI MAADUI LAKINI SI KWELI KUWA HAWANA NAFASI KATIKA UKUAJI WETU. Na huu ni mtazamo wangu, na yawezekana Namna Nionavyo Tatizo Ndio Tatizo
Lucky Dube katika wimbo wake wa Celebrate Life alisema tunaishi na wendawazimu wengi wenye nia tofauti. Kwenye The One akasema usiwape nafasi ya kukwambia "hili haliwezekani" maana "neno hilo halipo kichwani mwa jasiri" Msikilize hapa katika Celebrate Life nawe uwe Jasiri


BLESSINGS

4 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mmh, mi nimewashukuru kwani wamenipa changamoto kubwa sana.
Pia huwa nawaombea ili wasizidi kuziumiza hisia zangu wala kunikosesha amani.

Nakutakia siku mbili za mwisho zenye amani, furaha, upendo na mafanikio.

Yasinta Ngonyani said...

Mzee wa changamoto hiyo mbona sasa kali. Haya bwana nitawaombea wote na kuwashukuru.

Nakutakia pia wakati mzuri na uwe salama na uumalize mwaka 2008 vizuri.

Mzee wa Changamoto said...

Da Yasinta. Asante saaana saaana na nakutakia safari njema.

Yasinta Ngonyani said...

mzee wa changamotaasante sana kwa kunitakia safari njema. se u soon. bye