Thursday, January 22, 2009

Hivi marais wana dini ama imani?

Marekani
Sierra Leone
Nigeria
Zimbabwe
Honduras
Algeria
Phillipines

Nionapo marais wanavyokula viapo wakishika VITABU VITAKATIFU naishia kujiuliza kama wanafanya hivyo kwa kuwa wanaamini ama wanafuata taratibu. Najiuliza matendo ambayo huwa wanaruhusu na kuamrisha, miswada wanayosaini na "maslahi ya nchi" wanayolinda kisha najiuliza kama huwa wana dini ambazo wengi wetu huamini, ama wana imani ama "kawaida ni kama sheria"?
Labda ntahitaji msaada wenu wadau kujua hivi marais wana dini ama imani?


NB: Si nchi zote wanazotumia vitabu vitakatifu kuapa.

Wapo watumiao katiba na kitabu kitakatifu kwa pamoja kama Ukraine, wengine wakishika sehemu ya kifua ulipo moyo (kama Chile), wengine wakishika moyo na kona ya bendera (kama Hungary)wengine wakishikiwa vitabu vitakatifu juu ya vichwa vyao kama Indonesia
Pia wengine wanakula kiapo wakipiga saluti kwa picha kama China

5 comments:

Fadhy Mtanga said...

Sijui wanazo dini, siri yao mioyoni,
Sijui za utotoni, ama hivi ukubwani,
Sijui kama moyoni, wanayo kweli imani,
Nadhani hawana!

Mzee wa Changamoto said...

Asante Kaka Fadhy. Karibu tena nami nimekuwa na mtazamo wa hivyo. Kuwa pengine wanazo za utotoni maana maamuzi yao yantia shaka

Simon Kitururu said...

Vitabu , picha na ...washikavyo vina nguvu?

?

Subi Nukta said...

Niliposoma kichwa cha habari tu, kabla ya kujua maudhui, nilitabasamu kwa kuwa nilishaona mtizamo wako katika kuuliza swali hili. Ni sawa na kusema kuwa, umewaza sana na kwa kweli ungeambiwa uandike mawazo yako kutokana na habari hii, nafasi isingetosha. Ungeuliza, kama wana imani ni kwa nini huwa wanaiba?
Kama wana imani ni kwa nini wanakandamiza na kukubali ukandamizaji.
Kama wana imani na wanafahamu kuwa siku ya kiama inakuja, ni kwa nini wanaruhusu haki ipindishwe?
Kama wana imani ni kwa nini wana uchu wa madaraka?
Kama wana imani ni kwa nini wanaongopa wakati wa kampeni na wakishapata nafasi hawarudi kwa wananchi kuwaomba samahani kuwa walichodhania watakikuta huko kwenye uongozi sicho kilichopo na hivyo watashindwa kukamilisha ahadi zao?
Kama wana imani ni kwa nini wasikubali kupisha wengine kwa hiyari yao kuliko kung'ang'ania na kuendelea kuharibu zaidi na zaidi?

Hivi huyo wanayemuapia ama hicho wanachokiapia kwa imani zao, huwa wanajisifu kuwa emekula kobisi tu kiaina?

Anonymous said...

mpaka tutakapo elewa hili somo,ndipo tuta jua kwa nini sisi waafrica tuliacha kuendeleza imani zetu. nakwambia kitu kimoja it's a big secret kwanini mwenye nguvu ni mzungu na mwarabu na pia ndio wanao MILIKI UKRISTO NA UISLAM. labda na waafrica wangemiliki mila zao na kuziendeleza duniani kote! tunge kuwa like them by now HUWEZI ELEWA NI IMANI,ELIMU,UBUNIFU NAKADHALIKA. WE CAN ALWAYS DISCUSS TO GET CONCLUSION .THANX