Friday, January 2, 2009

Them, I & Them. ETANA:....Nothing But Love

"i say we owe nobody nothing but love, just love, sweet love. Straight from the heart" Hakuna ambaye anaweza kubisha kuwa kama kila mmoja ataliona hili, kama kila mmoja atatambua hili na kama mmoja atafanya hivi, basi ulimwengu utakuwa mahala pema sana pa kuishi kuliko ilivyo sasa. Etana, msanii ambaye katika mahojiano yake na website Jamaicans.com alisema jina lake lina asili ya kiswahili likimaanisha "The Strong One" (japo katika search yangu nimeishia waliposema ni la asili ya Afrika kwa maana hiyohiyo na bado naendelea) ameanza kwa kueleza aaminivyo kuhusu maisha yetu kama kila binadamu ataona umuhimu na nguvu ya UPENDO na ambavyo ama namna apendavyo maisha yawe mtaani akisema "as i take a little walk down the street, i nod my head to every single one i meet. Everytime i smile and say a BIG HELLO, don't you know, it is the only way to go? Cause we owe nobody Nothing but Love". Etana anaendelea kuongelea watoto akisema "as i watch the little children smile and plays, i wonder if there is a better way, cause their future is affected by today, so let us build a better place, for them to stay and play" Ndicho tunachohitaji tunapouanza mwaka huu wa 2009. Kuonesha upendo kwa watu wote, kujali watoto na kizazi kijacho kwa ujumla maana hakuna tunalodaiwa kulitenda maishani mwetu kwa wenzetu zaidi ya UPENDO.

Unaweza kuangalia mahojiano na "clips" za nyimbo zake zilizomo kwenye albamu yake ya kwanza na pekee alioipa jina Strong One ambapo humo kazungumzia ziara yake ya kwanza Africa, aliyoyaona huko ambayo hayaoneshwi kwenye Tv za huku, utu wa waAfrica na zawadi za kiAfrika ambazo hakuwahi kufikiria na sasa anajua. Bofya hapa chini

BLESSINGS
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.

IJUMAA NJEMA

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

what i love? define it please

Mzee wa Changamoto said...

Sijui wataka LOVE kwa mtazamo ama kwa nia gani? Yaweza kuwa na maana nyingi lakini pale inapofikia wakati wa kufikisha maana halisi basi ni lazima uambatanishe na maneno. Ndipo inapokuja lile suala la ku-define by reading the context na kama unaweza hilo utatambua ETANA alikuwa akimaanisha nini aliposema Love.
Mzee una changamoto weweeee???!
Blessings

Koero Mkundi said...

Upendo, I like that!

kaka Mubelwa kama dunia hii tuliyo nayo watu wangependana, tusinge shuhudia hivi vita vianvyorindima humu duniani,

Hebu angalia yanayotokea huko Israel, ambapo ndipo Ukristo unaosisitiza upendo miongoni mwa wanaadamu ulipoanzia, Iraq,Sudan,

Somalia na kwingineko, amani hakuna, watu hawapendani hawavumiliani.
Chuki zimetawala, watu wanajali fedha kuliko utu.

Kaka hii ni balaa, tunahitaji upendo utawale hii dunia ili tuepukane na haya majanga ya vita.