Wednesday, February 11, 2009

Afrika Kusini na vita dhidi ya VVU / Ukimwi

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Bi Barbara Hogan
Serikali ya Afrika Kusini imehidi kuongeza huduma yake kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi ambapo itaongeza huduma za madawa ya kurefusha maisha kwa waathirika wa virusi na wagonjwa wa ukimwi kutoka wagonjwa laki saba (700,000) wanaopata huduma hiyo kwa sasa mpaka milioni moja na nusu (1,500,000) ndani ya miaka mitatu ijayo.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Bi Barbara Hogan ambaye amekuwa mtetezi mkubwa wa waathirika na ambaye ameonesha kulipa uzito suala la Ukimwi ametangaza nia hiyo kama hatua kusaidia maelfu ya wananchi ambao wameathirika na virusi hivyo.
Afrika Kusini ndilo taifa lenye takwimu za waathirika wengizaidi wa Ukimwi ulimwenguni ambapo zaidi ya watu milioni 5.7 wanahofiwa kuwa na virusi vya ukimwi nchini humo ambapo takribani watu wapatao 1000 huhofiwa kufa kila siku kutokana na maradhi yahusianayo na Ukimwi. Gharama za kuwezesha kukabiliana na janga hilo kwa sasa nchini humo, zakadiriwa kufikia dola bilioni 25 kwa mwaka.
Waweza kubofya hapa kwa habari zaidi.
Changamoto yetu ni kujitahidi kuepusha maambukizi ya virusi hivi ambavyo kwa namba iliyofikia nchini Afrika Kusini (na hata nchini nyingi za kusini mwa Jangwa la sahara) ni ya kutisha na hiwezi kutegemea harakati na juhudi za serikali kutokomeza janga hili.
Ni vema na gharama nafuu kujilinda kuliko gharama za kujaribu kutibu na kutokomeza

2 comments:

Simon Kitururu said...

Umesema Mkuu, na kazi iko kwetu tu wapokeaji ujumbe tunafanyia nini ujumbe!

MARKUS MPANGALA said...

tuongeze ufunuo, kwani UKIMWI upo karibu yetu. Nilimaliza utafiti kuhusu ugonjwa huu mwezi januari, licha ya kwamba takwimu zimeshuka katika maambukizi lakini tabiza kuchochea maambukizi zinagonga mwamba