Thursday, April 2, 2009

Familia huishia wapi?

Tumezaliwa watano. Nina dada wakubwa waili na Kaka wadogo wawili. Yamaanisha ni mimi niliye kati. Na sina shaka kuwa wengi tutakubali kuwa hii ni familia. Na kama ambavyo nilishasema, nafurahia saana uhusiano tulio nao baina yetu. Lakini pia kuna Baba na Mama. Nao naamini tutawahesabu kama familia. Nao kila mmoja ana ndugu zake waliozaliwa pamoja. Hao kwao ni familia. Ni kwa mamtiki hiyo nahisi kuwa nao ni familia yetu maana ni familia ya sehemu ya familia yetu. Sasa mjomba na Shangazi wote si wana familia katika miji yao? Na hao ni familia za wazazi wetu na sisi na wazazi ni familia. Ina maana nisiwaite familia?
Najiuliza kama sisi sote si familia kwa mwendo huu na kama sivyo, basi basi naendelea kujiuliza kuwa hivi familia huishia wapi? Ama niseme mtu ni ndugu yako mpaka uzazi upi?

5 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ukiendekeza familia utaishia kwenye migongano na misuguano isiyoisha na uje kuchukiana na ndugu bure.

labda sisi sote ni familia moja japo unajiamba kuwa na familia pahala. mbele ya maumbile sisi tu wamoja na hivyo tu familia moja ndugu.

Amina

Yasinta Ngonyani said...

Kwa mimi familia ni wale tu niliozaliwa tumbo moja. yaani kaka, dada nk. Baba na mama sio familia yangu.Ni mawazo yangu!!

malkiory said...

Familia inategemea kulingina na jinsi unavyoainisha, kuna aina ya familia ambayo huhusisha baba, mama na watoto tu yaani nuclear family.

Aina ya pili ya familia ni hii inayoitwa extended family ambayo huhusisha wajomba, shangazi,babu, bibi, binamu nk

Siwezi sema ni aina ipi ni nzuri kuliko nyingine, faida na hasara zipo kwa kila aina ya familia, japokuwa kiwango cha faida na hasara hutegemea aina ya familia inayohusika.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

yasinta, wakati mwingine unahitajika ushahidi ili ujue kuwa kweli mlizaliwa tumbo moja au kutundikwa na uume mmoja. hili ni jambo la kiimani zaidi ya kisayansi bwana. nduguzo wote hunauhakika, bali uliambiwa na kuonyeshwa. hata babako huna uhakika ila unaamini kwa sababu ulijikuta ukimwita baba.


kwa hiyo basi, sisi sote tu wamoja na nifamilia moja yenye watu wa akili tofauti, rangi, tabia maumbo nk.

yaliyobaki ni anwani tu kuwa huyu ni dingi, maza, mume, dogo, nk

Albert Kissima said...

Familia inategemea sana na ukaribu.
Uliozaliwa nao umekua karibu nao kwa muda mrefu ndio ndio maana ufamilia unakuwa na nguvu kubwa.

Marafiki wanaweza kuishi pamoja kwa muda mrefu kiasi kwamba kila mmoja akahisi kuwa anaishi na ndugu wake wa kuzaliwa.

Shangazi na wajomba, hata babu na bibi unaweza kuwa wa familia yako kwani la msingi hapa ni ukaribu wako na ndugu hawa.
Hivi mtu akiishi na binamu yake kwa miaka mitatu mathalani, huyu si mwanafamilia?
Kwa hiyo mimi nadhani yeyote anaweza kuwa mwanafamilia ila ukaribu ndio jambo la msingi.