Tuesday, March 24, 2009

HAPPY BIRTHDAY SISTER Ninsy

Ndio. Ni mimi na Dadangu.
Naamini kuwa tunakuwa tulivyo kutokana na maisha tuliyopitia na pengine kwa ajili ya maisha yajayo. Lakini maisha tunayopitia tunakumbana na mengi na kukutana na wengi. Katika kukutana nao kuna hiari ya kuhusiana nao ama ulazima. Na inakuwa bahati mbaya pale ambapo unalazimika kuhusiana na mtu ambaye hudhani kuwa yuko pale kusaidiana nawe katika ukuaji wenu. Lakini ni BARAKA kuubwa kuwa na mtu ambaye kwa ulazima wa uhusiani wenu (yaani ndugu) anakuwa zaidi ya umtegemeaye, anakuwa rafiki na mtu ambaye kwako ni kama kimbilio la kile utakacho.
Nami nashukuru na kujivunia maisha yangu na wana ndugu wengi. Lakini zaidi ni hawa wa karibu na sitaacha kumsema ama kumtaja Dadangu Mkubwa Ninsy.
Ni dadangu mkubwa na ambaye niliishi naye miaka mitano ya mwisho niliyofululiza kuwa Tanzania na ninawiwa kusema kuwa bila yeye pengine ningekuwa mahala pengine na ama kuwa nilipo lakini kwa namna nyingine. Amekuwa mtu wa karibu saaana kwangu, ameni-support kuanzia kunisomesha fani ambayo mpaka sasa ndiyo inayonisaidia "kulisha minyoo" huku nilipo na pia kujiendeleza kwa namna nilivyo. Amekuwa mshauri pia katika mambo mengi na japokuwa kuna ambayo hatujawahi kukubaliana, lakini tumekubaliana kutokukubaliana na tunasonga kwa ubora na undugu zaidi.
Kwako Dada. Nakupenda saana, nakuthamini mno na pengine nafasi ya wazazi uliyoichukua imenifanya niwe nilivyo leo.
Nakutakia kila lililo jema katika maisha yako ambayo leo yanaanza mzunguko mwingine wa kalenda. NI SIKU MPYA ambayo mapambano kuelekea mafanikio yetu yanaanza na naamini na kuahidi kuwa msaada katika kila jema niwezalo utendalo.
Nakukumbuka na kukuombea saaana.
HAPPY BIRTH-DATE Sister Ninsy
Msikilize Luciano hapa akikwambia A New Day
"better days are coming, i can feel it in the wind....."
Love you Sis

15 comments:

Koero Mkundi said...

Kaka Mubelwa.

Hata mimi nasema Happy Birthday dada Nincy.
Duh! nimempenda sana dada yako, hakika ni mzurina anapendeza.
Nifikishie salaam zangu kwake.

Mzee wa Changamoto said...

Thanx K.
Ni dadangu na kama mzazi pia. Alinilea tena wakati uleee wa u-teenager. Sikuona kazi aliyokuwa nayo mpaka sasa nilivyoerevuka na kufikiria ujinga niliokuwa nao kichwani, natambua ni kazi gani alikuwa nayo kuniweka nilivyo lakini kwa namna aliyofanya.
Nampenda saana na pamoja na Dada ninayemfuata ambaye tumeishi wote tukiwa mbali na wazai, nawapenda na kuwathamini mno.
Natamani kama kungekuwa na maneno ya kusema zaidi ya haya K.
Ila naamini siku yaja ya wao kutambua thamani yao maishani mwangu.
Asante kwa kujiunga nami kumtakia siku hii K.
Blessings

Subi Nukta said...
This comment has been removed by the author.
Subi Nukta said...

Maisha marefu, afya njema na mafanikio bora yasiyopimika ndiyo ombi langu kwa ajili ya dada Nincy!
Mubelwa, umefunzwa heshima na adabu wewe ndiyo maana unaelewa maana ya shukrani na hata katika kukusoma kila ninakokuta alama zako, unatumia maneno mapole kufikisha ujumbe wako kwa hadhira.
Ufanikiwe katika mema yote!

Yasinta Ngonyani said...

Mubelwa, kweli una dada mzuri na pia ni kweli kumshukuru mungu kwa kukupa dada kama huyo. Na pia nakuomba kama hujamwambia/waambia ana kwa ana kuwa unawapenda na unawathamini sana. Fanya hivyo kama hujafanya.Nakuomba pia nifikishie ujumbe huu kwa dada Nincy:- Happy Birthday dada Nincy.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

basi bwana huyu dada nilikuwa nikikutana nae katika mazingira fulani ya chuo nilichokuwa nasoma hapa dar.

sasa siku moja usiku tumeenda uwanja wa ndege kumpokea binamu yangu kutoka states, mara namuona huyoo ila za ki-towm nikauchuna,nilishangaa kuona kwamba kumbe tulikuwa tunampokea mtu yule yule, basi ikawa mwanzo wa kufahamiana naye.

sijamcheki siku tele

hapy b'day ila kumbuka kusheherekea b'day ni kutukumusha kuwa kuna siku tutatoka na kuiacha miili yetu

Mzee wa Changamoto said...

Koero weye nshakwambia. Lol. Sa Subi nashukuru kwa sala za maisha mema na pia kwa mtazamo juu ya malezi ambayo ni matunda ya Dadangu mpenzi. Da Yasinta, asante tena na tena kwa kuendelea kuwa mshauri. Na ni kweli kuwa nimemueleza lakini ntaendelea kumueleza maana alichowekeza maishani mwangu ni kikubwa na najivunia kila siku. Kaka Kamala, hakuna ubishi juu ya maana ya kuongezeka kwa siku. Hakuna atakayebisha kuwa kila tunavyofanikiwa kusonga ndio tunavyofupisha mwendo wa huko tuendako (angalau kwa hatua hii) na hii ni changamoto yetu sote kujifikiria vema zaidi na kuishi maisha tuaminiyo kuwa ndio sahihi zaidi na kujiweka tayari kuuvua mwili huu.
Amani, Heshima na Upendo kwenu nyote

PASSION4FASHION.TZ said...

Happy birthday Nincy,mungu akupe maisha marefu zaidi na uendelee na moyo wa upendo kwa ndugu zako na kwa jamii inayokuzunguka.

Pili naomba nikupongeze wewe mzee wa Changamoto,kwa kuthamini mchango wake katika maisha yako, sio wote wenye moyo kama wako, naamini kuna wengi wamefanyiwa mengi na makubwa na ndugu zao kaka zao au dada zao lakini wanaona kama ni jukumu lao lazima wafanyiwe nawala hawathamini kabisa.

Anonymous said...

Happy B.Day Da Nicy.
Raha sana ukijua kupenda.
Upendo aliokupa na malezi aliyokupa itapendeza zaidi nawe ukatoa kwa wengine.

Anonymous said...

Afya njema na baraka kwa Dada Nincy. Pia hongera zake kwa malezi mazuri maana busara na heshima zako hazifichiki kila napoona kazi yako na kukumbuka kumshukuru dada yako ni ushuhuda tosha.Baada ya maneno haya naomba nikupe CHANGAMOTO (ukipata fursa)ya kuandika mawili matatu ambayo unafikiri ni muhimu kwa teenagers kufuata na walezi wa teenagers kuelewa (from teenagers' perspective)ili tuongezee kwenye hazina zetu sie tunaolea wadogo zetu.

Christian Bwaya said...

Hongera sana kaka Mube.
Mungu amekujalia dada mwema. Matunda ya malezi na nasaha zake zinadhihirishwa na hekima zako zilizo bayana. Wasomaji wa blogu hii ni mashahidi.

Wengine tunatamani bahati hiyo ingekuwa yetu (tunapojikuta tumewatangulia wadogo zetu), lakini haitoweza kuwa vinginevyo (kuitwa kaka ni changamoto).

Namtakia maisha marefu dadaetu. Maisha yenye kuwagusa wengi zaidi. Maisha yenye mafanikio. Namtakia kila liitwalo jema siku zote za maisha yake!

Umefanya vyema kumshukuru kwa mazuri alokutendea. Hilo hutendwa na wachache.

Ushauri wa Sophie uzingatie.

Anonymous said...

Inafurahisha kama nini kuona ubinadamu, wema, undugu na upendo vikitawala. Ni mambo mema kama haya yanayomfanya binadamu awe binadamu. Binafsi nimeguswa sana na maneno haya mazito ya Mubelwa kwa dadake mpendwa. Ni wazi kwamba dada Nincy alifanya kazi nzuri ya malezi kwani kwayo kumechomoza mti wa busara na matunda yake tunayaona hapa na kuyafaidi. Siku Njema ya kuzaliwa dada Nincy na Mungu aendelee kukubariki daima.

Mbele said...

Hongera sana, Mzee wa Changamoto. Picha ni nzuri sana na maneno yako yanagusa moyoni. Una bahati kuwa na dada kama huyo. Nawatakieni kila la heri.

malkiory said...

Mzee wa changamoto,

Hili limekuwa kweli changamoto hasa kwetu sisi ambao kwa namna moja au nyingine tumejisahau kuwakumbuka watu muhimu. Cheers and keep it up!

Mzee wa Changamoto said...

SHUKRANI SAAANA.
Ni busara unapoona watu wanajumuika nawe kusherehekea mafanikio ama hisia zako. Nami nawashukuru nyote kwa salamu, sala na maombi ya maisha mema kwa dada Ninsy. Ni vema kuwaeleza kuwa nawatakia vivyo hivyo kwenu na wapendwa wenu nyote.
Lakini pia niseme kuwa kazi aliyoifanya dada Ninsy na wanafamilia wengine (kuanzia wazazi na walezi wengine na hata ndugu wanipao changamoto za maisha) ilikuwa ni kuniandaa kwa namna ambavyo nitaweza kuishi na kujumuika na jamii fulani. Na hakika ni kazi yao hiyo inayonikutanisha na kunihusisha nanyi. Ninalomaanisha kuwa japo msingi ni mzuri, lakini hata huku juu mliko ninyi ambao nawasoma, nawaandikia na tunaandikiana na kusaidia kuerevuana ni mchango mkubwa saana wa kuwa nilivyo.
Hakuna hata mmoja wenu asiye na mchango katika maendeleo ya maisha yangu na wale nitegemeanao nao.
Kwa ufupi ni kuwa mzunguko wa maisha ni mkubwa, na uwepo wenu unakwenda kuwa msaada kwa hata wale msiowajua kama ambavyo msaada wa Dada Ninsy na ndugu wengine umenisaidia kuelimisha na kuisaidia jamii kupitia changamoto zetu.
Nawaheshimu na kuwatakia kila lililo jema.
AMANI KWENU