Monday, March 30, 2009

Matumizi mabaya ya pesa ni yapi?

Nimejiuliza maswali mawili kuhusu hili.
Kwanza ni kwanini watu wanapoongezewa kipato na matumizi yanaongezeka?
Kwanini watu haohao wanaweza kufanya mambo ambayo awali waliyaona ni anasa lakini kwa kuwa wanayamudu inakuwa sawia?

Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa na shida, akawa anahitaji pesa na alikuwa akilalamika kweli kuhusu ukata huo. Alipopata mahala pa kujikopa akawa anawahi huko akakamatwa na polisi na kutozwa faini. Ni kwa kuwa alikuwa na rekodi nzuri ya uendeshaji, askari akasema atamtoza faini tu na hatompa point kwenye rekodi yake. Rafiki yangu alifurahia hilo na pesa hiyo ambayo alikuwa akiiona haitoshi akaitumia kulipia faini hiyo.
Nikajiuliza kama kuna matumizi mabaya ya pesa ama ni utayari wa kutumia pesa tutakavyo?

2 comments:

Christian Bwaya said...

Tafakari nzuri Mube.

Kwa maoni yangu, fedha yenyewe haina maana yoyote isipokuwa inaponisaidia kupata kuridhika. Fedha ipo kuniwezesha kupata ridhiko. Kuridhika huja kwa kujisikia kuwa umepata ulivyovihitaji.

Kama nitaitumia fedha kupata ridhiko hilo ninalolihitaji (confortability), hayo kwangu ni matumizi sahihi, hata kama naweza kuridhika kwa kuonekana nimezitumia 'hovyo'.

Na mizizi ya ridhiko imo katika ufahamu zaidi, ambao waweza kuathiriwa na mambo mengi, ikiwamo ongezeko la kipato.

Kwamba kadiri ninavyoruhusu akili kudai mahitaji mengi zaidi ili niridhike, ndivyo ninavyochochewa kuzitafuta fedha zaidi na zaidi.

Kwa hiyo kwa jinsi hiyo, mzunguko waweza kukosa ukomo kiasi cha kufikia 'kutafuta hela ili uwape wengine' nk.

Ikiwa nitatumia fedha kinyume na dai la akili yangu, hayo yatakuwa matumizi mabaya. Kwa mfano pesa ambazo ningeweza kumpa mtu bure (nikajisikia kuridhika), nikajikuta nikizitumia katika matumizi mengine yanayoonekana mazuri (ila nikajisikia kutokuridhika kwa kufanya hivyo), hayo ni matumizi mabaya.

Ubaya ama usahihi wa matumizi, haupo katika fedha zenyewe bali katika kichwa (belief) cha mtumiaji mwenyewe.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Kila kondoo hula kulingana na urefu wa kamba yake!!!