Sunday, April 26, 2009

Labda hatuendelei kwa kuwa wa kutuendelesha hawako kwenye kiendesheo chetu (Prt 2)

Niliwahi kuandika kuwa hatuendelei kwa kuwa wenye mamlaka ya kutuwezesha kuendelea na / ama kutupa mwongozo wa kuendelea ndio wenye kutumia nafasi kunyonya na kufuja mali za wananchi.
Habari hii (bofya hapa kuisoma) toka NIPASHE ni kidhihirisho cha yale tuliyojadili hapa March 4. Lakini suala la Waziri mzima kushangaa kuwa kuna yanayotendeka kwa namna yanavyotendeka na kwa kiasi wanachotendeka, ni kipimo kingine cha UZEMBE na KUTOJALI kwa serikali na watendaji wake. Ni vigumu kuamini kuwa hakuna aliyekuwa akijua yanayoendelea mpaka waziri "ashitushwe" na matendo hayo.
Bado siasa inakuwa zaidi ya maslahi ya wananchi.
Ndio maana nakubaliana na Luciano aliposema Ulimwengu umejazana wale aliowaita BANDITS, ambao kwao tafsiri ya maisha inahusisha kuwatesa wanyonge na wenye uhitaji. Msikie anaposema "some of them claims they are boss, but all they do steal...... so much injustice, corruption in higher and low places......"


1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

kipande cha mziki nimekipenda sana na nakubalina. Ya kuwa ni kweli kana asiyeendelea hawezi kuendelesha wengine. jumapili njema