Thursday, April 23, 2009

Tatizo lipo ndani mwetu na si baina yetu

Moja kati ya nukuu bora nilizopata kusikia toka kwa Rais wa Marekani Mhe Barak Obama ni ile aliyosema kuwa "our destiny is not written for us, but by us."
Kutambua mustakabali wa maisha ni kutambua namna ya kuweza kuyafikia. Na kutambua namna ya kuufikia mustakabali wako basi wahitaji kujipanga vema na kujua kipi cha kufanya wakati gani ili kikupe matokeo gani na pengine kufikiria kuwa matokeo hayo yanaweza kuwa na changamoto gani zinazoambatana nazo.
Kwa ufupi, MAFANIKIO HALISI HAYAJI KWA KUKURUPUKA". Lakini bado kuna watuwenye imani kuwa tunaweza kuendelea kwa kuendesha maisha yetu kwa bahati nasibu. Yaani mwananchi anategemea maendeleo yaletwe na serikali inayoongozwa na watu wanaotegemea maendeleo yaletwe na nchi ambazo zinategemea kuendelea kuzikandamiza nchi nyingine ili zibaki kwenye "uongozi" wa ulimwengu.
TRazama sasa takribani miezi 18 kabla ya uchaguzi, hakuna ambaye ameanza angalau kuzunguka nchini kukusanya mahitaji na kuandaa ILANI ZA UCHAGUZI. Wanasubiri miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu waanze kumwaga pesa na kununua kura ambazo wakiingia madarakani wanajaribu wawezavyo kuzirejesha (pesa) na kisha kuwekeza nyingine ili uchaguzi ujao wasiende kukopa walikokopa sasa.
Lakini kwa bahati mbaya hakuna ayaonaye haya.
Hakuna ajiulizaye kwa nini waheshimiwa hawatambui mikataba feki mapema.
Hakuna ajiulizaye kwanini inachukua miaka kabla hujajua kuwa DECI ni feki.
Hakuna ajiulizaye kwanini hakuna anayefuatilia masuala muhimu ya wananchi.
NI KWA KUWA TUMEAMUA KUMEZA MATATIZO YETU NA KUWEKEZA JUHUDI KATIKA KUMSAKA ASIYEHUSIKA.
Mengi ya yanayotokea ni kwa kuwa tumeamua kuwa sehemu ya hayo ama "kwa kukusudia, au kwa kutotimiza wajibu"
Ni sisi wenye hatia, ni sisi wenye kuchagua wasiotujali, ni sisi wenye kukaa kimya bila kuhoji panapostahili, ni sisi tusioweza kujikomboa kwa kutochagua kwa kuangalia vigezo visivyofaa, ni sisi tunaokaa kimya tukishuhudia mali zikisafirishwa nje kiharamu, ni sisi tunaoshindwa kuwa na umoja kwa kuwa tu "tumenyamazishwa. ni sisi, ni sisi, ni sisi.
Nakumbuka Bob Marley alisema "emancipate yourself from mental slavery, none but ourselves can free our minds"

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unajaribu kumaliza tatizo kwa kuliongeza tatizo kama msemo wa blogu yako ulivyo kuwa uonavyo tatizo ndilo tatizo labda kuliko tatizo lenyewe.

yaani unawalauma majamaa fulani tu. unawalaumu wanaotegemea nje na wasiozunguka kuandaa sera japo utwambii wewe kama wewe ume/unafanya nini juu ya hilo uliitalo tatizo!

Mzee wa Changamoto said...

Duh!! We Kamala we!!! Anyway, nimesema sisi na ninaamini hata kuweza kusema ni hatua ya kwanza ili kucjhukua changamoto kama hii uitoayo. Kisha mimi nawe tunaweza kusonga zaidi ya hapa. Hivi ninaeleweka? Ok. Nadhani hii ni hatua ya kwanza kwangu na kwa wewe kuuliza ulivyoliza ni hatua nyingine na pengine mwingine atasoma na kufikiri na / ama kuweka wazo naye atakuwa amefanya hatua nyingine.
Kwa hiyo nashukuru kwa kuwa "sehemu" ya suluhisho.
Blessingssss

Koero Mkundi said...

Sisi watanzania aliyetuloga kafa na hata kaburi lake halijulikani lilipo......kazi ipo...

Simon Kitururu said...

''ni sisi, ni sisi, ni sisi.''

Umemaliza Kamanda.