Friday, April 10, 2009

Them, I & Them. ALPHA BLONDY.......Jerusalem


Tumekuwa tukionywa kutochanganya DINI na SIASA. Na hili lina ukweli kwa kuwa ni kama havichangamani. Lakini ukweli huu unashindwa kuwa halisi sehemu moja. JERUSALEM. Sehemu ambako siasa na dini vinaenda pamoja na kisha kuwa ni kitovu cha uasi unaoendelea kutokana na maamuzi ya kisiasa na kidini kwa dini zote kuu ulimwenguni.
Kunaonekana kutopata suluhisho la uhakika tangu kuanza kwa machafuko miaka ya 1940 ambayo yanaendelea kuua wengi na kutoonekana kupata suluhisho la kudumu zaidi ya utulivu wa muda mfupi kisha machafuko kuendelea. Da Koero aliwahi kuandika akiuliza HIVI KWA NINI TANGU MWAKA 1947 HADI LEO MGOGORO HUU HAUISHI? Bado machafuko yanaendelea kama ilivyoelezwa kwa kifupi hapa. Nyakati za utulivu kila mtu (mpenda mema na amani) hupafurahia. Na kati ya waliowahi kuonesha furaha ya kufika Jerusalem kukiwa na amani na kuona watu wa dini mbalimbali wakisali na kuishi pamoja kwa umoja ni Alpha Blondy ambaye aliamua kuimba wimbo maalum kwa heshima ya mji huo. Wimbo aliuita JERUSALEM na leo ndio tulio nao kwenye kipengele hiki cha I & Them
Fuatana naye katika wimbo huu uliorekodiwa nchini Jamaica mwaka 1986 akitumia bendi ya Bob Marley The Wailers. Bob ndiye alikuwa chachu ya Blondy kukacha elimu na kujikita kwenye muziki.
Msikilize.Alpha Blondy widget by 6L & Daxii
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

labada niliihsjibu kwenye makala yangu ya sisi niwamoja