Monday, May 11, 2009

Za Kale vs Maisha ya sasa.....MAMA WA KAMBO

Marehemu Hemed Maneti
Jana baadhi ya nchi walisherehekea siku ya kinamama duniani. Siku ambayo katika kusherehekea, niliamini tulitakiwa kuangalia tofauti ya thamani na maisha ya kinamama yalivyo sasa tukilinbganisha na yalivyokuwa miaka iliyopita.
Nami nilifanya hivyo kwa upeo na ufupi wa aisha yangu ambayo nimeweza kukumbuka. Na kati ya mambo ambayo naamini yanaanza kupiga hatua ni namna ambavyo kinamama wanaweza kusimama kujitetea na hata kutetewa na wenye kutambua haki zao. Hili linaendelea kuongezeka japo laenda kwa mwendo wa kinyonga.
Nakumbuka katika kukua kwangu nilishuhudia migongano mingi ya kifamilia iliyotokana na "mateso" ya mama wa kambo. Ni kweli kuwa wengi walikuwa wakitesa, japo wengi wa waliokuwa wakieleza hayo hawakupenda kueleza sababu za mateso hayo ama mwanzo wa yote.
Muziki wa leo katika kipengele chetu cha ZILIPENDWA unaeleza upande ambao Hemed Maneti akiwa na Vijana Jazz Band alisimulia. Msikilize kwa makini kutambua alichotambua juu ya Mama wa Kambo.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

6 comments:

Born 2 Suffer said...

Musee umenikumbusha mbaali sana yani hamna kama muziki wa zilipendwa, Ninazo album nyingi za zamani lakini hii nilikua sina asante kwa hichi kibao.

Yasinta Ngonyani said...

Kweli umesema akina mama wa kambo ni watu wabaya sana lakini sielewi kwa nini wanaroho ya kutu. Kwani wao wenyewe wamezaa halafu wanakuwa wakatili je wanauchungu tofauti? hata sielewi kabisa. Asante Mzee wa Cangamoto

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unawachukia akina mama wa kambo? mbona wengine wawakimbilia

Anonymous said...

hei. i don't understand your language actually. i really want to talk but idon't know where. so, i write it in here :D hey!! it's been a long time we haven't commenting each other! keep in touch mzee!!

Mzee wa Changamoto said...

Wala siwachukii hata kidogo. Nawapenda na ninalosema ni kuwa japo wapo waliokuwa wakitesa, hakuna aliyekuwa akijiuliza ni kwanini wnafikia hatua hiyo. Na hatua hiyo ilikuwa ikisababishwa na kitu fulani. Ninalosema hapa ni kuwa hawakuwa mataahira kuanza kutesa bila sababu, bali hakuna aliyesema walivyowachokoza mpaka wakaanza kuwatesa. NAWAPENDA, NAWAHESHIMU NA KUWATHAMINI SAANA kwani kama alivyosema Maneti, ni MAMA KAMA MAMA WENGINE.

Anonymous said...

Hujambo Mubelwa?
Kuna kazi inakusubiri. Pitia kwangu kwa maelezo.
Serina.