Tuesday, June 9, 2009

Ali Kiba ndani ya DC Metro

Leo nilikuwa napitia habari mbalimbali pamoja na sehemu za maonesho ya burudani ambako mara nyingi huwa napata ratiba za wanamuziki wa Reggae watembeleao miji ya karibu na DC na ambao mara nyingi huwa wanaanza kujipanga kwa maonesho nyakati hizi. Katika pitapita yangu nikakutana na tangazo la onesho lake Ali Kiba ambalo litafanyika ukumbi wa Zanzibar On The Waterfront

Nilifarijika saana kuona msanii huyu ameweza kufikia hatua ya kuandaliwa onesho mahala hapo ambapo pia wasanii wengi wenye kuheshimika hasa katika muziki wa kiafrika hufanya maonesho yao hapo. Nakumbuka onesho la mwisho mimi kuhudhuria hapo lilikuwa ni lake Oliver "Tuku" Mtukudzi ambaye sihitaji kumuwekea maelezo.
Nikaona ni vema kuwakumbusha wale wapenzi wa Ali Kiba kuwa atakuwa katika ukumbi mkubwa zaidi ya zile ambazo kina "anonymous" wamekuwa wakiziita kumbi za Birthday.
Lakini pia nikawiwa kuwakumbusha wahudhuriaji kuwa hawaendi kumuona Ali Kiba akitumbuiza na wao kumtolea macho, wajitahidi kushirikiana naye katika kucheza. Mimi kama msanii (japo wa "level" ya chini) najisikia vibaya nionapo msanii anatumbuiza na ni yeye pekee anayewajibika ilhali wengine wamemtumbulia macho.
Tazama onesho la Ali Kiba lililofanyika hapa DC ambalo asilimia kubwa ya wahudhuriaji wahudhuriaji walikuwa wakimuangalia kama hawamjui ama hawam-feel ama hawaelewi kiimbwacho wakati naamini wimbo ulioimbwa ni kati ya nyimbo zake maarufu.

Jamani JICHANGANYENI NA MCHEZE NAYE BASIII MKIENDA HAPO Zanzibar O.T.W

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Aisee hapo kazi kwelikweli!!!!