Saturday, June 27, 2009

Give it all you've got today

Ndimi naye.
Tangu nikiwa mdogo nilielezwa kuwa si kila kitu chatendeka katika mfumo wa ku-"save the best for the last." Na nilielezwa kuwa wakati mwingine unaweza kufika last kabla hujapata nafasi ya kuonesha the best yako. Nimeliona na kujikuta mhanga wa hili. Mambo mengi yametokea ambayo nilitamani kama ningetambua mapema na kuonesha namna ninavyojali. Najua si mimi pekee, bali watu wengi wamekuwa wakijuta kutokuwa wazi kwa wenzao ambao hundoka bila taaria / maandalizi na hivyo kuwaachia pengo la kuueleza umati na si wao namna walivyokuwa wakiwathamini watu hao. Ndio maana siku zote najaribu kueleza hisia zangu kwa yule anayefanya vema na kunisaidia katika ukuaji wangu.
Wiki hii rafiki yangu Dr Msia Kibona-Clark anahama hapa DC Metro kwenda kuanza kazi mpya na bora zaidi katika chuo kikuu kilichopo jimbo jingine mbali na hapa. Dr Msia amekuwa si rafiki kwangu bali pia msaada kwangu na "familia" yangu. Japo tulikutana na kuongea mengi pale tulipoweza na japo alinieleza mpango wa kuhama muda mrefu kiasi, bado sikuweza kutumia kila nafasi niliyokuwa nayo kuonesha thamani ya mema mengi aliyonionesha, kunisaidia na kuniwezesha.
"Lakini popote uendapo ntakumbuka, kuthamini na kuendeleza yale mema niliyojifunza toka kwako, kwani hiyo zaidi ya changamoto yangu pekee, bali ni CHANGAMOTO YETU sote."
Mtabibu, mwanafalsala, mwanamuziki na mwanatheolojia Albert Schweitzer alisema "At times our own light goes out and is rekindled by a spark from another person. Each of us has cause to think with deep gratitude of those who have lighted the flame within us."
Thank you Sia and Stay Blessed
Nililojifunza ni kuwa, jaribu kutenda kila uwezalo kwa yule umthaminiye kwani si kila mtu hupata nafasi hiyo na wakati mwingine unapofika wakati wa mwenzako kuondoka, nafasi ya kumdhihirishia umthaminivyo hukosekana kabisa kulingana na mchakato wa maisha ulivyo sasa. Fanya kama alivyosema Beres Hammond. Just Give it all you've got (today)

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mubelwa kwa kweli umefanya vizuri si watu wengi wanafanya ulivyofanya. Mungu azidi kukupa nguvu uzidi kuongeza hiyo hali.

Anonymous said...

Mzee una marafiki kweli. Na unawashukuru kila siku. Naona hata wengine watajifunza.Umeandika kweli sometimes tunasubiri mpaka mtu afe ndio tuseme alikuwa muhimu

Fadhy Mtanga said...

Kaka, nilipofika mwishoni katika kusoma post yako, niliduwaa kwa muda kiasi nikijaribu kufikiri mambo mawili matatu. Nimekumbuka makosa kama hayo. Mwaka jana mwezi Machi nilimpoteza mwalimu na rafiki yangu mkubwa. Katika kufahamiana kwetu, sikuwahi kumwambia bayana kiasi nilivyomthamini na kumwona muhimu katika maisha yangu. Alipoondoka ghafla. Nikatamani angeamka nimwambie namna pengo lake lisivyoweza kuzibika. Mungu amrehemu.
Nimejifunza, kupitia hapa. Nakubali, hata nami napaswa kufanya hivi kabla wakati haujanitupa mkono na kunifanya kushindwa kumfikishia ujumbe mlengwa mwenyewe.
Ahsante mara lukuki kwa changamoto hii.
Wikend njema.

PASSION4FASHION.TZ said...

Kaka Mubelwa,wewe ni mfano wa kuigwa,wewe ni mtu mwenye hekima,busara na mstarabu sana,kila nikipita hapa kwako najifunza kitu, na popote napokuta kuna maoni umeweka kwenye blog nyingine huwa ni yahekima na busara,hakika umebarikiwa na mungu azidi kukubariki na kukuongoza,natamani kama ningekuwa naishi karibu na wewe,hapana natamani kama ungekuwa ni kaka yangu, hapana natamani kama ungekuwa ni mshauri wangu mkuu!!hakika hapo kichwa kipo hongera sana, zaidi ziende kwa dada mkubwa aliyekulea.

Mzee wa Changamoto said...

Wow!! Mwanzo nilihisi itakuwa too much kuweka hisia zangu kuhusu watu walionisaidia maishani, lakini niliona ni vema nikasema ili watambue kuwa sehemu ya ukuaji wangu inatokana na juhudi zao. Ndio maana nikaweka kipengele hiki cha Jungu Kuu ambacho najitahidi kuwaenzi wale wote walionifanya niwe nilivyo (japo wengine wako kwenye kipengele cha Greetings)
Napenda kuwashukuru ninyi mnaotembelea hapa, mnaotoa maoni kila iitwayo leo na mnaosoma na kupata moja mawili ya kutumia ulimwenguni. Nami najifunza saana kutoka kwenu.
Dada Yasinta unatambua michango ya hawa ndugu. Nawe usiye na jina asante saana kwa kuacha yaliyo moyoni. Kaka Fadhy, heshima kwako, pole kwa kumkosa huyo aliyekutendea mema na naamini aliko anatambua na kuona uenzi wako. Dada Schola!! Natamani kungekuwa na neno zaidi ya asante kwa maneno yako. Na nashukuru kuwa umewashukuru wale walioniwezesha kuwa hapa. Kwa hilo nasema ASANTENI NYOTE na naamini tutaendelea kufunzana jinsi siku zinavyosonga.
Blessings

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nadhani kila mmoja wetu ameshawahi kuguswa kwa namna moja au nyingine na jambo hili. Siye kama binadamu wakati mwingine tunachukulia mambo kijuu juu tu na kusahau kwamba hapa duniani maisha yetu hayatabiriki. Mimi babangu mdogo aliyehakikisha kwamba nasoma aliondoka kwa ghafla tu wakati ndiyo nimekuja huku kuanza masomo. Yaani sikuwahi hata kusema asante ya kweli; na mpaka leo nikimkumbuka huwa najuta kweli. Kila siku inabidi tuishi kama vile ndiyo siku yetu ya mwisho - tukiwaenzi na kuwashukuru waliosaidia katika kutufikisha hapa tulipo.

Mija Shija Sayi said...

Hakuna kitu muhimu ktk maisha yetu kama msingi(foundation). Msingi wa maisha mtoto anaoupata kwa wazazi wake ndiyo hujenga au kubomoa maisha yake akiwa mtu mzima na ndiyo hutathmini tabia ya mtu. Kaka Mubelwa tabia yako ya "uthaminifu" nina hakika haijakurupuka tu, ninaamini kabisa ni mchango wa wazazi wako ndiyo sababu tabia hii haikutoki.

Kama watu wote tungekuwa na tabia ya kuthamini na kumweleza muhusika uthamani wake, basi kusingekuwa na stress duniani(narudi kule kule kaka yangu mambo ya kudili na stress)hakuna kitu kinatia faraja kama unapofanya jambo zuri halafu mpokeaji wa jambo hilo akalipokea kwa heshima, shukrani na kukili kwa mdomo wake, huwa inatia nguvu na raha hata kama una stress huondoka na mwamko mpya huja.

Watu tujifunze kutoka kwako, shukrani za kimya kimya hazifai na wala hazijengi.

Ubarikiwe mzee wetu wa changamoto, kila la heri kwa DR. pia.

Mbele said...

Mzee wa Changamoto

Shukrani kwa taarifa hii. Baada ya kuisoma, nimeenda hima kutafuta habari za huyu mwalimu Msia Kibona-Clark, na nimeona kuwa anafanya utafiti unaofanana sana na wangu, juu ya tofauti zilizopo katika fikra na tamaduni baina ya waAfrika na waMarekani. Anayoandika kuhusu uhusiano wa waMarekani weusi na sisi waSwahili yanafanana na yale ambayo nimeyabaini na kuyataja katika maandishi yangu.

Inaleta faraja kuona kuwa unachokigundua katika utafiti kinafanana na kile walichogundua wengine pia.

Pamoja na shukrani zangu kwako Mzee wa Changamoto, namtakia kila la heri mwalimu Msia Kibona-Clark.