Sunday, June 28, 2009

Give Thanks and Praises..COME DOWN FATHER by Luciano

Ulimwengu hauoneshi kwenda ambako wengi wamekuwa wakitarajia. Na wala hauonekani kuwa mahala pema tena pa kuishi. Beres Hammond aliimba akisema "i see greedy and i see selfishness every man is for himself, only you can talk to them Father cause they listen to no one else"
Ndivyo ilivyo sasa. Ni vita kila kukicha, ni dhuluma kila mahali, mauaji na ukatili kama sehemu ya maisha na mateso kwa kinamama na watoto vyawa sehemu ya maisha yao ya kila siku.
Naye Luciano anaimba katika wimbo wake huu kuhusu mambo mengi ambayo yamebadilika na ambayo haamini kama kuna anayeweza kuamini kuwa yanatendeka. Anaeleza kuhusu maradhi, vita, kubadilika kwa nyoyo za wanadamu na mengine mengi.
Analofanya ni KUMUOMBA MUNGU arejee na kuokoa ulimwengu maana wengi hawana mwelekeo wa kubadilika.
Msikilize Luciano katika nwimbo huu COME DOWN FATHER
JUMAPILI NJEMA

3 comments:

chib said...

Aameeen

Yasinta Ngonyani said...

Jumapili njema kwako na pia familia yako. Ubarikiwe sana .

Nicky Mwangoka said...

Shukrani mkuu.Thanks and Praise forever and ever.Amen