Tuesday, June 23, 2009

Kama huu ndio upendo wao kwa nchi, basi tuchague wasiozipenda

Katuni hii ya GADO na nimeikuta kwenye baraza la Dr Faustine na kupenda maelezo yake. Dr kaandika
Ha ha ha! I found this interesting Gado cartoon in the Kenyan Daily Nation showing G40, a club of stolen elections... I am sure you identify some members of this club.
Membership to this club is limited to greedy, selfish and power hungry ruling elite. The club vision is "to be the only ruler until death". The mission of the club is "weed out potential successors and create a family dynasty" and the motto is "Power at all costs".
Nimekuwa nikijiuliza yanayoikumba dunia sasa hivi. Kisha nakumbuka makala ya Kaka Fadhy Mtanga aliyoandika kuanisha jinsi alivyoona namna wanasiasa walivyo walipo kwa maslahi yao nikajiuliza mengi.
Najiuliza huu upendo wa nchi anaokuwa nao Rais ambaye haamini kuwa kuna mwingine anayeweza kuiongoza nchi hiyo kama yeye na matokeo yake kung'ang'ania urais mpaka afe unatoka wapi?
Najiuliza hawa wanasiasa wanaosema wanaipenda nchi na kuamuru mambo yanayosababisha wananchi kuua, kuuawa ama kufa wanazungumzia upendo wa namna gani?
Najiuliza hawa wanasiasa wanaozipenda nchi zao kiasi cha kutaka kubadili katiba ili waendelee kutawala hata baada ya kuishiwa uwezo wa kutawala wanatoa wapi upendo huo?
Nimesikia kila aitwaye MUASI anavyojitetea kuwa yupo pale alipo ili kutetea maisha na mali za wananchi. Kila aitwaye muasi anasema anapigania nchi yake aipendayo, na kila aliye madarakani anagoma hata kutoka kwa kuwa anaipenda nchi yake.
Ni upendo gani huu walionao wenzetu?
Ule upendo wa nchi ambao utamuwezesha kuiba akiwa madarakani na kisha kutumia sehemu ya pesa anayotuhumiwa kuiba kujiwekea dhamana?
Upendo wa nchi utakaomuwezesha kuipindisha katiba na kuiba na kisha kutoshitakiwa kwa kuwa katiba aliyoivunja wakati akiiba hairuhusu kuvunjwa kumtia hatiani?
Ule upendo wa nchi wa kujirundikia mali na kukosa wa kukuwajibisha kwa kuwa madaraka si ya mfumo wa kisheria namna hiyo?
Upendo wa wengi wa wanasiasa si wa haki. Upendo wa wanasiasa wengi si wa kuwajali wananchi na upendo wao si kwa maendeleo ya wananchi. Nilimsoma Kaka Kamala kwenye maoni ya Prof Matondo juu ya TULICHOJIFUNZA TOKA KWA ZE UTAMU ambapo alisema "labda ianzishwe ze uchungu" na ninaamini alimaanisha kuanzishwa kitakachokuwa kinyume na ze utamu. Nimewaza mantiki hiyo na kuhisi KAMA HUU NDIO UPENDO WA WANASIASA KWA NCHI ZAO, BASI TUCHAGUE WASIOZIPENDA NCHI ZAO.
Labda wataachia ngazi baada ya muda wao wa kikatiba kuisha, labda hawatang'ang'ania madaraka wakiona watu wao wanakufa kwa maradhi na njaa, labda hawatapenda mianya ya rushwa na ufisadi, labda hawatabebana na labda watafanya kinyume na haya tuyaonayo sasa.
BLESSINGS

3 comments:

Simon Kitururu said...

Kazi kwelikweli!:-(

Fadhy Mtanga said...

Unajua nini kaka? Hawa watu wawili muhimu sana katika kipindi cha mvuvumko (Renaissance) huko Italia, karne ya 15 na 16, Niccolò di Bernardo dei Machiavelli (1469-1527) na The Prince wake Cesare Borgia (1475-1507) ndiyo walioacha makovu haya.
Viongozi wanafuata sana kanuni za Niccolò Machaivelli, aliyewafundisha namna ya kufanya ili kutawala muda mrefu.

Ni hayo tu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

siku hizi naandika makala katika jarida la rai.

labda nitazitundika kwenye blog ili tusaidiane kupata chanzo cha tatizo