

Bendi hiyo yenye tabia ya kupelekana mchaka mchaka na washabiki wa mziki ughaibuni inatarajiwa kutumbuiza majira ya saa 10.00 alasiri,ambako washabiki wa nyimbo za kiswahili na mziki wa dansi wanaisubiri kwa hamu bendi hiyo, iliyofanikiwa kujizolea umaarufu kwa kutumia mdundo wa dansi wa bongo.
Kiongozi wa bendi hiyo Ebrahim Makunja aka Ras Makunja ataliongoza kundi hilo jukwaani kwa kazi moja tu nayo ni kuwadatisha akili washabiki! Wasikilize kwa kubofya www.myspace.com/thengomaafrica ama waweza kuwasiliana nao kwa barua pepe kupitia anwani ngoma4u@googlemail.com. Kujua mengi kuhusu kundi hili mahiri, bofya hapa
http://www.africa-news.eu/news/entertainment/the-ngoma-africa-band-continues-to-thrill-fans.html
Source: Msema Kweli
No comments:
Post a Comment