Zamani migongano ya kifamilia ilikuwa ya kifamilia na ilisuluhishwa na wanafamilia zaidi. Heshima baina ya wanafamilia ilionekana kuwa kubwa kuliko sasa, na hata masuluhisho miongoni mwa wanafamilia nayo ilikuwa ya ndani. Sasa hivi mambo yamebadilika na sina hakika kama ni maendeleo ama la, lakini bado naamini MAMBO YA NDANI YANASTAHILI KUBAKI NDANI (japo yategemea ndani kukoje).
Leo katika kipengele hiki tunao DDC Mlimani Park wana Sikinde Ngoma ya Ukae ambao chini yake Cosmas Thobias Chidumule wanaeleza walivyosuluhisha "mgogoro" uliopo kati ya kaka ya Chudumule na Mke wa Kakaye huyo.
Burudika ukijifunza.** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**
4 comments:
Ni wimbo mzuri wenye mafunzo mazuri! Asante kwa sahani hii yenye ujumbe murua.
Nimeupata ujumbe huu nimefurahi sana.asante
mimi nilipata amani, na utulivu baada ya kutoa matatizo yangu nje ya familia. nikaishia kujitambua na yale yoote niliyoyaona kama amatatizo yakawa vichekesho na vifurahishio vyangu, yaani??? we acha tuu
mambo ya ndani yanastahili kubaki ndani... inategemea ni jambo lipi... wala sio familia.
Post a Comment