Monday, June 8, 2009

Za Kale vs Maisha ya Sasa....NAJIBU TELEGRAM

Maisha yetu yanabadilika jinsi tukuavyo. Yanabadilika na kubadilisha mfumo mzima wa maisha. Tuliongelea namna ambavyo DUNIA IMANI IMEKWISHA na kuisha kwa imani huku ndiko kunakotulazimisha kuishi kwa msaada wa "fulani" ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Tunahitaji jicho la ziada kwa karibu kila kitu tufanyacho. Kusaini chochote, kununua chochote na hata kusuluhisha kitu sasa ni tofauti na zamani.
Zamani migongano ya kifamilia ilikuwa ya kifamilia na ilisuluhishwa na wanafamilia zaidi. Heshima baina ya wanafamilia ilionekana kuwa kubwa kuliko sasa, na hata masuluhisho miongoni mwa wanafamilia nayo ilikuwa ya ndani. Sasa hivi mambo yamebadilika na sina hakika kama ni maendeleo ama la, lakini bado naamini MAMBO YA NDANI YANASTAHILI KUBAKI NDANI (japo yategemea ndani kukoje).
Leo katika kipengele hiki tunao DDC Mlimani Park wana Sikinde Ngoma ya Ukae ambao chini yake Cosmas Thobias Chidumule wanaeleza walivyosuluhisha "mgogoro" uliopo kati ya kaka ya Chudumule na Mke wa Kakaye huyo.
Burudika ukijifunza.

** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

4 comments:

Anonymous said...

Ni wimbo mzuri wenye mafunzo mazuri! Asante kwa sahani hii yenye ujumbe murua.

Yasinta Ngonyani said...

Nimeupata ujumbe huu nimefurahi sana.asante

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nilipata amani, na utulivu baada ya kutoa matatizo yangu nje ya familia. nikaishia kujitambua na yale yoote niliyoyaona kama amatatizo yakawa vichekesho na vifurahishio vyangu, yaani??? we acha tuu

Anonymous said...

mambo ya ndani yanastahili kubaki ndani... inategemea ni jambo lipi... wala sio familia.