Friday, June 12, 2009

Them, I & Them...RIVERSIDE...........Culture

Hapa ndio RIVERSIDE kwangu. Ninapopatumia ku-edit Video na Picha mbalimbali, kuwasiliana na wapendwa mbalimbali, kusoma blogs na mambo mbalimbali, kusikiliza miziki mbalimbali na pia "kurusha" CHANGAMOTO mbalimbali. Umeshagundua Riverside yako?

Dunia imekumbwa na hali mbaya ya uchumi ambayo inasababisha watu kushindwa kuzikabili hasira na kupoteza ubinadamu na kutenda yasiyotendeka kwa kuwa tu uchumi umewafanya waishi waishivyo. Juzi tumesikia kuhusu mtu aliyeingia makumbusho ya Holocost hapa Washington DC na kuanza kufyatua risasi zilizoua na sababu zikiwa ni chuki za kibaguzi na pia akilalamikia kumong'onyoka kwa mafao yake ya uzeeni (Soma habari yake hapa) . Jamaa alipata stress na hakujua pa kuzitua. Kaishia kufanya maafa. Pengine nyimbo kama hizi ni dawa muafaka
Da Mija kwenye Jamvi lake ameeleza wimbo huu kama "The song that lift me up when i'm down." Na mimi nikakubaliana naye moja kwa moja. Na si tu kwa kuwa naupenda wimbo huu, bali kwa kuwa mafunzo yaliyomo ndani yake ni ya KITAMBUZI zaidi. Culture anaimba zaidi kuhusu kujitambua na kutambua wapi panaweza kuwa sehemu ya kuondolea msongo wa mawazo (stress) ambazo zimekuwa chanzo cha maafa mengi duniani hasa nyakati hizi za kuharibika kwa uchumi na maisha kwa ujumla. Yeye ansema huenda kando ya mto lakini wewe waweza kwenda ama kufanya jambo jingine.
Kwa kujua lilipo pumziko la stress zetu, tutaepuka maafa mengi na hata kuepuka maradhi yaletwayo na stress hizi na hivyo kuifanya jamii kuwa na furaha hata wakati wa shida.
Ni Utambuzi, Utambuzi, utambuzi wa kujitambua (kama nilivyoeleza HAPA) utakaotuwezesha kurejesha utu na kuishi kwa furaha.
Msikilize na / ama kumtazama Culture katika wimbo huu huku ukisoma "lyrics" zake kumfuatilia kwa zaidi.
Waweza msikilize hapa chini (wimbo waanza sekunde ya kumi na sauti ni ya chini kiasi)

Ama mwangalie hapa chini

For I woke on Saturday morning
Feeling sticky and dirty after work
Took a walk down a riverside

I roll a little spliff
Sat down on a stone and start to cool off
With my burden down a riverside

For I check around the youths
And I try to teach the truth
Lay their burden on the riverside

I walk through every corner
Try to find someone to talk to but I have to
Lay their burden on the riverside

For I walk and I talk
And I linger and I search
Lay their burden on the riverside

And I walk, I met the youthman pocket
And I try to search around them
Lay their burden on the riverside

And I sat down quietly
Watch the fishes circle around the little stones
Lay their burden on the riverside

I cup my ears and I heard the little birds
Whistling in the tree like so
Lay their burden on the riverside

Live good among your neighbor
Like sister and brother and
Come with me a riverside

All you need is pray to Jah, quality
You see secret shall be revealed
Lay their burden on the riverside

(solo)

Jah provides for the birds in the air
And the fishes in the sea so what about me
Lay their burden on the riverside

Look at the crow they toil not neither do they spin
Yet father provide far them
Lay their burden on the riverside

Let us walk and talk
And pray quietly in search
Lay their burden on the riverside

Look at the color of those clothes, oh Jah
Make each and every one individually
Lay their burden on the riverside

Where is the love?
Where is the togetherness too?
Lay their burden on the riverside

I can't take the war and I can't take the shooting
Neither the looting, just
Lay their burden on the riverside

I tried around Rema
Even in The Jungle
To find a quiet rest

Round there in a Nannyville
My heart come to a trail
Lay their burden on the riverside

And I knock, and I search
And I whisper and I preach
Lay their burden on the riverside

Where is the quietness
And the love to be found in some corner?
Lay their burden on the riverside

Let us walk, let us search
Let us examine and let us see
Lay their burden on the riverside.


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Shukrani Da Subi kwa wimbo na Da Mija kwa maneno. UPENDO DAIMA

5 comments:

Anonymous said...

Kaka nakubaliana na ujumbe wako.
Unajuwa katika kitengo maalumu cha River side kuna mambo mengi muhimu sana.Je mabepari wanaweza kuwa na riverside?

Rasta hapa.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio. kwenda mtoni kunarleta pumziko na amani. kwingini ni porini, kwenye kijua cha asubuhi na jioni au milimani, kutembelea eneo jipya nk. waweza pia kwenda beach na kusikiliza sauti za maji, sauti za ndege, miti nk vinginevyo ni meditation tu

Yasinta Ngonyani said...

hapo naona pametulia. Ijumaa njema nawe Mubelwa!!!

Anonymous said...

KI UKWELI NI KUWA UNANIGUSA SANA NA MAMBO AMBAYO UMEKUWA UKIYATOA KAMA CHANGAMOTO KATIKA KIOTA CHETU WADAU SITAKI KUSEMA LOLOTE ZAIDI YA KUKUPONGEZA NA KUWA TUPO PAMOJA KAKA SANA TU.. MALKIA SOPHIA HAPA

Simon Kitururu said...

Sina cha kuongezea zaidi ya kutamani kutembelea Riverside yako siku moja. AMEN!