Wednesday, July 15, 2009

Ndiko yalikoanzia?????

Nilipoandika kuhusu kifo cha Michael Jackson, Kaka Kamala aliniomba kama ningeweza kupata habari kuhusu kujibadili kwake na kushirikiana nanyi.
Pamoja na kusubiri matokeo ya mwisho ya vipimo vya kitaalamu kuhusu kifo cha Michael Jackson, bado kifo chake kinahusishwa zaidi na madawa ya kupunguza maumivu ambayo alionekana kuyatumia kwa muda mrefu na kuwa addicted nayo. Ni hakika kuwa sasa wapo wanaoamini kuwa uchunguzi unaoendelea sasa ni kujua nani alimpa madawa hayo, alistahili kupewa madawa hayo na ni kwa kiwango na usimamizi gani alikuwa akiyatumia kwani wapo wanaosema kuwa walionya juu ya matumizi ya madawa hayo.
Lakini pia zipo habari kuhusu mwanzo wa matumizi ya madawa hayo na hata kichocheo kingine cha kubadilika kwa ngozi yake. Na hiyo inasemekana ilitokana na kuungua wakati akitengeneza tangazo la Pepsi kama inavyooneshwa katika video hii iliyotoka punde.
Yasemekana baada ya kuungua alianza kutumia madawa makali ya kupunguza maumivu na pengine ndio mwanzo wa matumizi mabaya ya madawa hayo. Na wapo wahusishao hili na mabadiliko yake ya muonekano wa ngozi. Tukio lenyewe la kuungua ni hili hapa kama lilivyotolewa na US Weekly

1 comment:

Anonymous said...

Aliungua vibaya sana sana aisee, kama ni hii, basi kweli aliungua na kuumia. kupata 2nd na 3rd degree burn si mchezo na inavyelekea kweli alipata 3rd degree burn kwa kuwa ile huunguza neva ambazo ni mishipa ya fahamu hivyo huwezi kusikia wala kuhisi maumivu yoyote hadi mtu anayekuona unaungua akuambie. Marehemu Babu yangu alifariki kwa 3rd degree burns, hadi anafikishwa hospitali, yeye anadai arudishwe nyumbani, haelewi ni kwa nini wamemwamsha kutoka usingizini, kwa kweli kumwona alivyokuwa ameungua mgongoni, ilibidi kumlaza kwa tumbo, yeye haelewi ni kwa nini, ndipo utaomba imani, alifariki siku chache baadaye! Burn wounds si mchezo na ni ngumu kweli kutibika, hasa ikiwa ni 2nd wachilia mbali 3rd degree burn! Si mchezo.