Wednesday, July 15, 2009

Space Shuttle Endeavour yaondoka salama

Endeavour ikiondoka toka launching pad 39 A ya
Kennedy SPace Center. Florida
Baada ya kuahirishwa mara 5, hatimaye Space Shuttle Endeavour imeweza kuondoka na kufika kwenye Orbit bila kuonesha matatizo yoyote. Japo itachukua muda wa ziada kwa wataalamu kuzisoma video zilizochukuliwa wakati wa kupaa kujua kama kuna hatari athari zozote zilizotokea wakati wa kuondoka na pia kusubiri uchunguzi wa awali kuona kama kuna hatari yoyote kwenye shuttle hiyo.
Endeavour itakuwa kwenye space station kwa siku 16 kumalizia ujenzi wa maabara ya kiJapani.
Binafsi ni "mlevi" wa mambo ya Space na nayapenda na kuyafuatilia saana (unakumbuka nilivyorejea kutoka "shamba" nikaeleza kuhusu Dr Don Thomas ambaye ameshakwenda huko kwenye space station mara nne? Jikumbushe HAPA). Ukitaka kuona jinsi ilivyo raha (na hatari vilevile) hebu angalia zinavyoondoka katika video hii hapa chini ya Shuttle ya mwisho kuelekea huko Space station mwezi wa tano mwaka huu.

Ama waweza kuangalia hapa jinsi Space Shuttle Endeavour ilivyokuwa ikifanya mzunguko wa kuwawezesha wataalamu kuikagua kama kuna hatari yoyote na kisha uone inavyotia nanga katika Space Station

Ama pia waweza kuangalia moja ya SPACE WALKS walizofanya waliokwenda huko mara ya mwisho kufanya ukarabati wa Hubble

Ama nilipokwenda kwenye makumbusho ya mambo ya anga na kujionea moja ya Space Shuttle zilizowahi kwenda huko kwenye Space Station na kurejea salama. Ni Space Shuttle Enterprise

No comments: