Sunday, July 26, 2009

Nyota mwingine auawa. Ni Vernon "The Vipe" Forrest

Tulikuwa tukijiandaa kushuhudia mpambano wa mkongwe huyu wa ndondi wiki ijayo (Aug 1)ambapo alitegemewa kutoa upinzani mkali na pengine kuibuka mshindi dhidi ya Sergio Martinez, lakini hilo halitatokea kwani Forrest ameuawa jana katika jaribio la kumpora gari lake aina ya Jaguar.
Licha ya kuwa katika timu ya taifa ya Marekani iliyoshiriki Olympic mwaka 1992 na pia kuwa bingwa wa WBC uzito wa Super Walterweight, Forrest anakumbukwa zaidi kwa mapambano yake mawili dhidi ya Shane "Sugar" Mosley ambapo alishinda yote na Sep 18 mwaka jana alitwa mkanda wa WBC uzito wa paundi 154 lakini alinyang'anywa mwezi may mwaka huu baada ya kushindwa kuutetea kutokana na maumivu ya mbavu. Mpaka mauti yanamkuta, Forrest alikuwa na rekodi ya kushinda mapambano 41, kupoteza 3 na kutoka sare 1 na alishinda mapambano 29 kwa knockout.
Forrest anaongeza orodha ya wanamichezo maarufu waliouawa katika siku za karibuni na kuacha utata wa mwisho wa maisha yao. Habari za nyota wengine waliofariki karibuni (na pengine kiutata)BOFYA HAPA
Taarifa zaidi toka ESPN ni hii hapa chini

REST IN PEACE "THE VIPE"

2 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mungu airehemu roho yake. Amen.

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Habari za kusikitisha! Masumbwi ndiyo mchezo wangu (nina sababu zangu), na hivi karibuni umekumbwa na mfululizo wa maafa mf. Arturo "Thunder" Gatti na sasa Vernon "The Vipe" Forrest". Nililitazama pambano lake na Sugar Shane Mosley na japo hakutegemewa kushinda kwani wakati ule Mosley ndiye alikuwa "Manny Pacquiao" - best pound for pound. Alimchakaza Sugar vibaya sana na tangu wakati ule watu walianza kumuona kama mmoja wa wapiganaji wazuri kabisa. Mungu ampumzishe salama!