Tunapoangalia namna ambavyo nchi zetu za Africa (hasa TANZANIA) zaendeshwa, tunaweza kujiuliza kama tunajua sisi ni nani, tunaelekea wapi na pengine tunahitaji nini kufika kule tutakako.
Ni kitu kibaya saana kuwa na WATAWALA (wenyewe wanajiita viongozi) ambao wanaonekana kutawala nchi kwa kujilimbikizia kile kipatikanacho na ambacho kingekuwa kwa manufaa ya wananchi lakini wao wanavigeuza "chao". Tunashuhudia namna ambavyo viongozi wetu hawajali watu wao, hawajali afya, maisha na ubora wa maisha ya waTanzania. Kwao si juu ya yale afanyayo mTanzania, bali ambayo wanaweza kuyatumia toka kwa mTanzania kupata watakacho. Yaani wengi ni HYPOCRITES. Wanaongelea UPENDO usiokuwepo (kama nilivyoandika hapa), wanaongelea AMANI wakati ndio wanaosababisha vita kisha wanakwenda kwenye mikutano "ya amani" na kula pesa tu (kama ilivyoandikwa hapa).
Tunajiibia wenyewe ( kashfa za UFISADI & EPA), tunajihujumu wenyewe (MATARUMA YA RELI nk), tunajidhalilisha kwa kutowathamini waTanzania wenzetu na kuwapa "wawekezaji" haki hata ya kuwamwagia sumu wananchi.
HIVI SISI TUNAFAA WAPI?
Tunazidi kujipoteza katika kupenda kujilimbikizia yale ambayo hatuwezi kuwa nayo milele na tunafikia hatua ambayo hata wasioona wanasikitikia wasikiacho ndani ya AFRIKA.
Leo hii barani Afrika kiongozi kuondoka madarakani baada ya muda wake kuisha anapongezwa (kwa kuwa wanategemewa kungang'ania madaraka) na wale wanaoingia kinguvu (kama Sudan, Uganda na kwingine) wanaendelea kung'ang'ania madaraka wakiamini hakuna mwingine anayeweza kufanya (japo) karibu ya kile wafanyacho.
KWANI SISI WA-AFRIKA TU WATU WA WAPI NA TWAFAA WAPI?
Sikiliza wimbo huu ambao umeimbwa kwa kuchanganywa na mahadhi na maneno ya kiZulu. Hakika ni wa kiAfrika, toka kwa mwanaAfrika kuwauliza waAfrika.
Sikiliza WHERE WE BELONG? toka kwake Nasio Fontaine (msome hapa)
Intro....
African (Zulu)
Vocal riffs (ancenstral callings)
Dae Dn, Dae-e-yeah! Yeaheh!
Long live Ithiopia
Oh ho uuh!!!
Blackaman, Blackman
Where is your country?
Where is your King?
Ho! Ho! Ho! Where is your Nation?
Where is your GOD?
Chorus
You fe look upon land Ithiopia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Nubia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Africa,
Where we belong?
You fe look upon land of Ithiopia
Where, where we belong?
Who uuhh!
Blackaman, Blackman
There is NO JUSTICE,
BLIND MAN AND ALL CAN TELL YA
There is NO PEACE
Hoh! Hoh! Hoh!
There is NO FREEDOM
While LIVING IN CAPTIVITY,
So don't mek (let) them fool ya
Chorus
You fe look upon land Ithiopia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Nubia,
Where we belong?
You fe look upon the land of Africa,
Where, where, where, we belong?
You fe look upon land of Ithiopia
Where, where we belong?
Blackaman, Blackman
Where is your country?
Where is your King?
Ho! Ho! Ho! Where is your Nation?
Where is your GOD?
Chorus x4
**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Ni kweli inasikitisha lakini pia kwa nini tunachagua viongozi waiofaaa?
yasinta labda na wachaguaji hawafai!!!!
mnapoongelea matatizo ya Tz Gusia kwa kiasi kikubwa dini kwani zinachangia kutuduwaza!!!!!
Dada Yasinta, mara nyingi wale wanaogombea huwa hatuwajui undani wao, mara nyingi huwa tunaridhika na maneno matamu na sera za kuchongwa ambazo kiuhalisia wala hazitekelezeki.
Ili tupate viongozi walio bora,mbali na sera zao lakini ni vema sana kama tutafuatilia utendaji kazi wa watu hawa kama walishakuwa viongozi na kama hawakuwa viongozi basi namna wanavyoishi na jamii.
Post a Comment