Thursday, September 10, 2009

Unamlaumu Kanumba???? Kwani alimuwakilisha naniiiii???

Juzi juzi "nyota" wa maigizo Tanzania Steve Kanumba aliteuliwa / chaguliwa kwenda kuungana na "nyota" wengine katika siku ya kwanza ya Big Brother Africa. Huko alionekana na kuongea na baada ya hapo, watu wamesema meeengi kuhusu yeye (na mimi nilikuwa mmoja wao "waliochonga") lakini baadae nilipoendelea kufuatilia mjadala huu hapa nikawaza. HIVI KANUMBA ALIMUWAKILISHA NANI??? Aliwakilisha kundi la wasomi wachache waTanzania ama kundi la walio wengi wenye elimu ya kati (tena iliyo katika mfumo m'bovu wa kikoloni"?) Waliomponda wengi wao ni wale "waliosoma" ama wale wanaoishi nje ya nchi ambao nina hakika kuwa hawako kundi moja na Kanumba. Kanumba alimuwakilisha kijana halisi wa kitanzania ambaye amekulia mazingira ya kusota na kujiwekezea katika juhudi za kazi (na kashfa kiasi) kukuza jina lake. Na kwa hakika kama hili kundi ndilo ambalo Kanumba anapatikana basi tujiulize ushiriki wake kulingana na hawa "wenzake". Si la wale ambao kwa mihangaiko yao ama ya wawawezeshao (usisahau ufisadi) wameweza kwenda kusoma na kujua "this and that". Ni mwakilishi wa kundi letu sisi ambao serikali imetusahau na kutojishughulisha nasi kisha inataka kuja kujivunia sifa za wachache wetu wanaobahatika kufanikiwa. Si unaijua tena Tanzania yangu. Ivunayo isipopanda (bofya)
Kama Kanumba anawakilisha mamilioni ya vijana wa kiTanzania ambao wana elimu kama yake, unadhani unaweza kumuweka na vijana wanapi ambao wataweza kukaa nyuma ya Camera na kuongea kama alivyoongea??? (muulizeni Candy na "weekly address" zake awaambie ilivyo ngumu). Na pengine kwa mazingira aliyosomea, kukulia na hata afanyiayo kazi, tulitaraji Kanumba awe na kingereza cha kiwango gani?? Mbona tupo wengi wenye kiwango hicho na tunawaona wengi hata nchi za nje (kama hapa Marekani) ambao wametoka kwao (mfano waMexico) na kuishi hapa miongo kadhaa na bado hawezi kuunganisha sentensi? Ni kweli kuwa Kanumba kafanya vibaya namna hiyo na si kwamba kuna sababu ya ziada kumshambulia? DaMdogo Candy katika "ulimwengu wake mdogo" ameuliza kwanini watu wengine wako hivi?? (Bofya hapa kumsoma) na japo ilikuwa kabla hili "halijalipuka", lakini na "walewale" kina sie aliokuwa akijiuliza.
Kanumba alifanya alivyofanya na ni kwa "nguvu zake mwenyewe" bila msaada wa ziada. Labda angeweza kufanya vema zaidi kama angepitia njia njema zaidi lakini hakupitia. Na si yeye tu apitiaye alikopitia, bali ni wengi tunaopitishwa huko.
Kwa kundi ninaloamini kuwa Kanumba yumo, na kwa namna alivyoongea (kulinganisha na kundi alilomo) nadhani anastahili kutolaumiwa. Bali kupongezwa na kisha kujua kuwa sasa amanza kwenda nje ya ulingo ambao anajihisi kuwa huru na kuelekea ulingo ambao lugha yaweza kuwa kikwazo na sababu ya "wanoknok" kumkatisha tamaa. Wengi wa wasemao wasingeweza kufanya alivyofanya. Kwetu tunasema "na atabaase asheka" (hata ambaye hawezi kufanya kile ufanyacho, atakucheka ukionekana umekosea).
Kuna mengi ya kujifunza Kaka Kanumba lakini haimaanishi kuwa unastahili kubeba lawama. Tambua ulipoanguka (kama unahisi umeanguka) kisha songa mbele, na "next ijayo" ukiwa hewani watakuali mabadiliko nawe utajivunia mafanikio. Nelson Mandela alisema "the greatest glory in living lies not in never falling, but in rising everytime we fall"
Your Greatest Glory is on your way Brother.
Kama hukumuona unaweza kupata vipande viwili vifupi hapa BONGO CELEBRITY.
Bado niko shamba. Nikipata cha kurejea nacho ntakujuvya. Tuonane Next Ijayo

8 comments:

Albert Kissima said...

Binadamu yeyote anahitaji kupewa moyo pale anapoanguka ili aweze kuinuka na hatimaye aweze kusonga mbele.Lawama na masimango havina maana kwani si suluhisho la ufanisi wa mtu.



Wenzetu wa Magharibi nadhani wanautamaduni tofauti kidogo kwani pale mtu anaposhindwa hazomewi, hachekwi bali utaona anashangiliwa na kupewa moyo.Huku kwetu bwana, leo Taifa stars imefanya vizuri, Maximo anasifiwa kweli kweli, kesho imefurunda, watu wanasema hafai, sasa kwa hali kama hizi sidhani kama tutakaa tuyakubali na kuyathamini yale wayafanyayo wengine hata kama yana upungufu wa hapa na pale.

Bennet said...

Kwa upande wangu mimi sijaona tatizo kuwakilishwa na Kanumba ingawa mimi sio mpenzi wa sinema zake kabisa
Kwa ufupi Kanumba ni supastar wa kiTanzania kwa maana ya supastar halisi aliyepitia msoto wa kibongo, shule kama Kayumba wa haki elimu na alianzia kuigiza kwenye maigizo mpaka sasa kapata mafanikio kidogo na anaigiza hizo wanazoziita sinema.

Kuna waliolaumu kwamba hajui kiingereza, sawa yeye ni mTanzania na anakijua kiswahili vizuri kama lugha yake ya taifa, shule aliishia form 6 pale jitegemee, sasa ukichukulia kwamba alisomea mkoani wapi sijui na dar alikuja alipofika sekondari kwa hiyo utakuta kiingereza ni lugha yake ya 3 ukianzia na lugha ya alikokulia
NInachoweza kumshauri Kanumba ni kwamba asilewe na mafanikio aliyoyapata aongeze bidii na arudi shule hata kama ni masomo ya jioni na ikiwezekana hii sanaa ya maigizo aiendee shule kabisa

chib said...

Kama candy alivyosema, wabongo ni waoshwa vinywa, ha ha haa

Fadhy Mtanga said...

Tunawashukuru sana Google kwa mapinduzi ya Blog sasa tunasema hisia zetu. Kaka Mubelwa, naomba nikiri wazi, mimi ingawa sikuwa mwosha kinywa, nafsini mwangu nilikuwa na mtazamo hasi juu ya uwakilishi wa Kanumba. Ni mmoja ya waliodhani tofauti. Sikutazama show, pilika zilinitinga. Lakini niliposoma post yako, nimejaribu kufikiri kwa marefu na mapana. Nilikosea.

Mi ni mtazamaji wa muvi za Kanumba. Ingawa zina makosa fulani, bado namkubali Kanumba kama mpambanaji asiyechoka. Na hilo nalikubali. Na kwa kutambua hilo nikaenda pale kibarazani 'Diwani ya Fadhili' na kuandika shairi 'Usichoke'
Hivyo nampa moyo SK, asichoke, apambane vilivyo.

Kanumba, tukubali tusikubali ni mmoja ya alama muhimu katika mapinduzi ya sanaa ya filamu Tanzania.
Tanzania sasa inapitia Rennaissance katika film industry. Mmoja ya wanamvuvuko wa mwamko-sanaa katika uigizaji ni Kanumba.
Nampongeza kwa hilo.

Ushauri wangu, awe msikivu. Awe mwepesi kujifunza kutokana na changamoto mbalimbali azipatazo. Apende kusoma vitabu mbalimbali kutoka kwa waandishi mbalimbali ili kukuza uelewa katika kiwango cha juu zaidi.
Naamini yupo juu, na atakuwa juu zaidi akiwa na silaha kuu tatu: VISION, MISSION na TARGET.

Viva Kanumba, Viva sanaa ya filamu Tanzania.

Ni hayo tu.!

shamim a.k.a Zeze said...

HAKIKA umeongelea kitu kimenigusa, baada ya kusoma hapa nikajaribu kuvaa viatu vya Kanumba, nikajikuta ingekuwa mule mule

kwani last year alienda mdada mwenzetu Latoya, nae alikuja akanangwaaaaaaaa, wakati alichokifanya hakuna kigebi as long as alikuwa ndani ya jumba hilo ambalo ni sehemu ya mchezo, kwani kuna kina dada wenzie akiwemo kina abby, ofuneka hata walitembea na wanaume humo humo

hivyo ni waosha vinywa tu hakuna jinsi ya kutukwepa.....nina uhakika kabisa kati ya hao wanaosema tukiwabeba kuwapeleka itakuwa hivi hivi tena na zaidi ya kanumba uchemfu watakoufanya

kuna watangazaji wa redio clouds, wameweka hadi jingle ya kumponda , nika uhakika tukimchukua mmoja wao tukamtupa kule INGEKUWA NI ZE COMEDY

SO WACHA TUIPOTEZEEEE

shukran changamoto cos umenipa changamoto....nimeandika saana eee wink!!

zeze alipita hapa leo

Anonymous said...

Hatukatai Mzee wa Changamoto na wengineo ,DSTV kumpeleka Kanumba ni sawa ila watu wanashindwa kujieleza swali ni hiv English ya Kanumba ni Bado hata kama sio Lugha yetu mbona mwisho,Richard na latoya walikuwa wanaelewa maswali Siku ya Ufunguzi aliiingia Diary Session Kanumba aliuzwa hiv akajibu Opposite jamani hata kama tunataka Macelebrity wako Watangazaji wazuri Kina Emel Chris wa Choice Fm ,Ruben Ndege aka Ncha kali wa Clouds ,Seven wa MTV ,Penny wa Channel Ten ,Jokate ,basi si wangempeleka basi Miss Africa Nancy Sumari jamni,People lets be seious sio mnasema tuuu Watanzania bwana halafu kesho yake twapiga kelele.

Mzee wa Changamoto said...

Kwanza nilete SHUKRANI ZANGU ZA DHATI kwa nyote mliotumia muda wenu kuacha mawazo mema. Nashukuru kwa uelewa na tafakari zenu na kubwa HESHIMA na BUSARA toka maonini mwenu.
Kwa kaka Anon (usiye na jina) wewe nakushukuru zaidi kwa kuwa wengi wasiopenda kutambulika huamua kujibu visivyo kwa kuwa hakuna atakayewajua. Lakini wewe licha ya kutokubaliana nasi moja kwa moja, umeendelea kuheshimu kibaraza.
Ulivyosema ni kweli kuwa wapo wengi ambao wangeweza kuongea vema kiingereza na kuwakilisha kuliko Kanumba. Lakini bado najiuliza kama hao wangekuwa wanawakilisha waTanzania ambao wako kundi moja na Kanumba. Mimi hapa sisemi kuwa Kanumba hana la kujifunza. Ninaamini kuwa alijifunza mapeeema na pengine kabla hajaanza kuongea. Na kuna ambayo hata yeye moyoni mwake anatamani asingeyasema vile ama angesema zaidi, lakini ndio kujifunza huko.
Pia kuhusu mifano iliyotajwa sijui kama iko "level" moja kimaisha na Kanumba. Namaanisha kuwa kina M.L Chris nimesikia maisha yao. Sidhani kama wako kundi moja la "makuzi" na sisi.
Lakini pia sidhani kama kuteuliwa kwa Kanumba badala ya uliwatoa kama mifano ni kosa la Kanumba na si multichoice wenyewe. Kama waliteua na kisha wakajua kuwa kunahitaji brush, basi wangefanya hivyo. Lakini kama hawakufanya basi asilaumiwe Kanumba.
Na kama aliambiwa akaona ni ngumu kiasi lakini akaamini kuwa ataweza kupambana na majaribu haya, nampongeza zaidi kwani hii ndio njia pekee ya kujijua ulipo na kuji-challenge. Kumbuka tulivyoaswa na Robert Fritz kuwa "If you limit your choices only to what seems possible or reasonable, you disconnect yourself from what you truly want, and all that is left is a compromise."
Kwa mara nyingine ASANTE SANA NA KARIBU TENA

Faith S Hilary said...

Heheheh chib!! Mie sisemi mengi maana I ran out of water ya kuosha huo mdomo hicho kinywa.