Wengi wanamfahamu kama Mpiga Besi mahiri nchini Tanzania ambaye anatumbuiza na kuelimisha akiwa na bendi ya The Kilimanjaro Band (Wana Njenje / Kinyaunyau). Wenye kumfahamu zaidi wanamfahamu kwa utaalamu wake wa kupanga sauti na kama mmoja wa sound engineers wakali zaidi nchini.
Wengine wanamfahamu kama mtayarishaji mahiri wa muziki (Producer) pale Njenje Studio Ilala na wapo wanamfahamu kama mzazi na mlezi.
Sina hakika ni wengi wanamfahamu kama nimfahamuvyo mimi. Kumfahamu Kepi Kiombile kama MWALIMU aliyenielimisha meengi kuhusu muziki na utayarishaji wake.
Ilinzaje??
Ilinzaje??
Mwaka 2002 nikiwa Times Fm nilifanya mahojiano na msanii mmoja wa muziki wa asili na baada ya mahojiano hayo, mkuu wa vipindi Master T akaniita na kunipongeza kwa kipindi kisha akasema kwa upande mwingine nilishindwa kuuliza maswali mengi ambayo alitaraji na akanipa mifano ya maswali hayo. Kwangu yakawa ya kiufundi zaidi na nilisikitika kutoyafikiria. Lakini ukweli ulikuwa wazi kwamba sikuwa na ujuzi wa ndani wa muziki huo wa asili. Kwa kuwa ndio nilianza mahusiano ya kikazi na kundi la Muziki wa Asili la SISI TAMBALA "wana Ngwashala", nikaungana nao (Sisi Tambala) kuelekea Studio za Njenje walipokuwa wakirekodi kuweza kujua machache kuhusu utayarishaji, kurekodi, magumu na mepesi wakabilianayo wasanii wakiwa studio. Nikakutana na watayarishaji kama Kepi, Samweli Luhende, Saghati na mwingine ambao walinipokea vema. Nilikuwa na muda mwingi na Kepi ambaye ni kama alinilea na kunionesha mengi kuhusu muziki na kwa hakika nilijifunza mengi na baada ya hapo hata maswali yangu na uchambuzi wa muziki vilikuwa vya ki-ufundi zaidi kuhusu sanaa ya muziki.
Almanusura nianze kujifunza muziki na nilianza kuwa "comfortable" na mazingira ya studio na hata kutoa ushauri kwa wasanii kadhaa waliokuwa wakirekodi wakati nikiwa pale. Ilikuwa ni baraka kubwa.
Pengine CHANGAMOTO YETU kubwa ni kukubali makosa na kisha kutafuta namna ya kuyafanya kama uzoefu wa kujifunzia (learning experience) na hiyo itatuwezesha kuwa waangalifu na makini zaidi katika kazi. Ni katika kuisaka ELIMU HIYO YA MAPUNGUFU yaliyoonwa na Master T nikakutana na Kaka Kepi ambaye ni zaidi ya mwanamuziki, zaidi ya mtayarishaji wa muziki, zaidi ya mtaalamu wa sauti, zaidi ya fundi mitambo, zaidi ya mzazi na mlezi kwani pia ni MWALIMU KWA CHIPUKIZI KAMA SISI.

ASANTE SAANA KAKA KEPI
Moja kati ya kazi nilizoshuhudia zikirekodiwa ni hii yao Sisi Tambala (kabla kina Ashimba, Dr Kumpeneka, Naima na wengine hawajalihama) ambayo inaitwa KATOPE. Sikiliza muziki halisi wa kiTanzania uliorekodiwa kwa umakini wa hali ya juu. Gitaa zito limejazwa naye huyohuyo Kepi.
2 comments:
kama mtayarishaji na mtangazaji mchanga wa muziki wa kiafrika nlipata nafasi ya kufanya mahojiano na KEPI katika kipindi cha afrika bambataa na kubaini ni hazina kubwa ya muziki barani afrika, VIVA KEPI, VIVA AFRIKA.
Watu wote tungekuwa tunawakumbuka waliotusaidia kufika tulipo, kweli waliotoa mchango wa mafanikio yetu wangekuwa wanajisikia fahari ya namna yake.
Mie nampa hongera zake nyingi sana tu
Post a Comment