Saturday, October 24, 2009

"Tumetokomeza Malaria visiwani Zanzibar"...Waziri Asha Juma

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imesema kuwa imeweza kutokomeza maradhi ya Malaria katika visiwa hivyo. Hayo yalinenwa na Waziri wa Kazi maendeleo ya vijana, wanawake na watoto wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe Asha A. Juma wakati akizungumza katika sherehe za tano za kila mwaka za shirika lisilo la kiserikali la SHINA INC* zilizofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita hapa Maryland.
Waziri Asha Juma ambaye ndiye aliyekuwa msemaji mkuu mwalikwa usiku huo alisema kuwa wameweza kutokomeza ugonjwa huo unaoua watu wengi zaidi barani Afrika kwa msaada mkubwa wa serikali ya Marekani. Amesema kuwa kutokomeza malaria ni kati ya mipango iliyokuwa katika MILLENIUM DEVELOPMENT GOALS (MDG) ambayo yalihusisha mambo 8, kama anavyoeleza kwenye hotuba yake pamoja na namna ambavyo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakabiliana na kufanikiwa katika hayo
Baada ya hotuba hiyo, blogu hii ilipata nafasi ya kuhojiana na Mhe Waziri Asha kujua kwa kina kilichofanyika Zanzibar kutokomeza Malaria ambacho hakiwezi kufanyika Bara ambako ugonjwa huo unaendelea kuua maelfu. Pia kuhusu suala zima la usahihi wa takwimu na afya za wanawake na watoto.


Sherehe hizo zilipambwa na burudani toka kwa kikundi cha vijana cha Taratibu cha hapa Washington DC na pia kwaya ya K.K.K.T Bukoba. Pata sehemu ya burudani hiyo


Kwa habari na picha zaidi waweza kuBOFYA HAPA na / ama HAPA

*SHINA INC ni shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kuwasaidia VIJANA, WANAWAKE NA WATOTO wenye uhitaji kwa kuwawezesha kimitaji, kielimu na hata kufadhili watoto yatima na wale waishio katika mazingira magumu. Waweza kutembelea tovuti yao kwa kuBOFYA HAPA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nimeiona hii Shina na nimekuwa nikiangalia mwenendo wake na watu inaowaasaidia na kujiuliza maswali meeengi bila majibu.
labda nikae kimya kwa sababu shirika hili linaongozwa na ndugu (shangazi) yangu wa kifamilia na labda ili kulinda amani na mshikamano wa kifaamilia (kama kweli upo) naona nisiseme chochote hapa au nipongezi (kinafiki) juhudi za shirika hilo ili nionekane mwanafamilia bora.

ukifuatilia majina ya kiongoza wa shirika hili utagundua kuwa kuna jina Kamala likithibitisha mambo fulani ya undugu wa duniani. HONGERENI KWA KUSAIDIA YATIMA JAMAI NA ENDELEZENI MOYO HUO NA MUNGU HAWATANGULIA - Amina !!!!!?????

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaa Kamala.
Ameeen

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Kamala unaniangusha mwanaharakati wangu.

Wanaharakati wakiogopa mjomba au shangazi tutafika kweli?

Hebu tuweke tathimini yako kuhusu SHINA...

Tufafika tu.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndaki, hatupaswi kusababisha negatives kama tunaweza kuziepuka