Friday, November 27, 2009

Tanzania Yangu.....Iliyo "bize" kumwagilia matawi badala ya mizizi


NAJUA LEO NI IJUMAA NA NILISTAHILI KUBANDIKA TOKA LABEL YA I & THEM LAKINI NAOMBA NIIZUNGUMZIE TANZANIA YANGU
Katika beti ya kwanza ya wimbo wake GUNS & ROSES, Lucky Dube aliimba "I don' t know why I keep believing that one day they' ll bring us together. When they' ve shown in more ways than one that all they care about is the dollar"
Ndilo ninalowaza sasa kuhusu WANASIASA wa nchini mwangu Tanzania ambao wanaonekana kutojiandaa kwa lolote jema wanalotaka kufanya.
Bwawa la uzalishaji umeme la Kidatu Image from http://www.industcards.com/hydro-africa.htm. Bwawa la uzalishaji umeme la Kihansi Image from http://www.industcards.com/hydro-africa.htm.
Nimemsikia Rais Kikwete bila aibu akiwaalika wawekezaji huko Jamaica wakati waTanzania wana mgao wa umeme unaozidi nusu ya siku yao.

Angalia uwiano wa ubora baiskeli na mavazi na viatu. Na bado twategemea kwenda Olimpiki. Image from http://www.issamichuzi.blogspot.com/
Rais wangu huyohuyo anazungumzia mafanikio ya michezo ya Jamaica na kuyataka Tanzania ilhali wamefuta michezo mashuleni na hata iliyopo haina viwango wala usawa

Taswira za Polisi Msimbazi... Yaani Dar Es Salaam katikati ya jiji. Sijui mikoani kukoje
Kweli mtu aishi kwenye magofu haya na bado aipende kazi wakati "mafisadi" wanaishi kama wako nusu peponi?? Picha toka http://mtwarakumekucha.blogspot.com/
Ninasikia wakisema kutokomeza uhalifu na kutaka askari kuwa waadilifu ilhali maisha ya nyumbani kwao yako hivi.

Ndiyo mazingira yatuzungukayo hayo na kuna Halmashauri zinazotukata kodi. Askari wa jiji wanaokimbiza na kupora Mama ntilie na Machinga wasisimamie usafi. Picha toka http://mtwarakumekucha.blogspot.com/

Twawasikia wakizungumzia AFYA YA MLAJI na kuzungumzia kuboresha afya ya mtanzania na urefu wa maisha yake. Lakini utekelezaji ndio huo tuuonao. Yaaniiii.............

Hawa ndio viongozi wetu wa kesho. Lord Have Mercy. Picha toka Michuzi Jr blog na Mch. Emmanuel Bwatta kupitia Adam L. wa blogu ya http://www.upole.blogspot.com/

Na mwisho twasikia mpango wa Kompyuta kwa wote japo twajua hata ubao wa kuandikia una utata. Hakuna ukuta na hata ezekeo ni la ajabu. Hakuna viti wala madawati na nina wasiwasi kama waalimu ofisi zao si nyumbani mwao.
Ninachojiuliza hapa ni kwanini Rais na viongozi wengine waanze kushughulikia kuhusu UWEKEZAJI wakati hata Barabara, Maegesho na mitaro ya maji taka haijajengwa? Kuleta wawekezaji ilhali wasomi hawapo nyumbani ni sawa na kuwaambia wawekezaji kuwa WATATAWALA MILELE kwani hakuna atakayekuja kuchukua nafasi yao.
Kwanini tusiboreshe Makazi ya Askari, Kwanini tusihakikishe wanafunzi wote wanasoma katika mazingira yanayowapa muda wa kufikiria masomo na mazingira ya masomo?
Wamekaa wakiwekeza kwenye kumwagilia matawi huko kwenye vikao waendako ilhali mizizi ya hapa nyumbani inakauka.
HAWATAFANIKIWA KAMWE kwani wanamwagilia kisicho sahihi.

Tanzania Yangu ni kipengele kinachozungumzia ytale yaendeleayo nchini Tanzania na namna ambavyo "ndivyo sivyo" inavyozidi kupamba moto nchini. Kwa matoleo yaliyotangulia BOFYA HAPA
Tuonane "Next Ijayo"


4 comments:

Sisulu said...

mada tete inasisimua mjadala mkubwa lakini niseme kuelekea mabadiliko mbinu nyingi zinatumika wataalamu wanamshauri raisi ili wamfurahishe na sio kumfurahisha mtanzania wa kawaida aliyeku songambele tabora au aliyeko chisolya majita musoma vijijini. hivyo mabadiliko ya kweli yatakuwa marefu kuyafikia. hoja nzuri. zidumu fikra- mageuzi

Bennet said...

Hili ndio naona tatizo la viongozi wetu, nashauri Raisi angaeamua kuanza na vitu vichache muhimu kutokana na ulazima wake mfano aanze na maji, umeme, barabara na kufufua bandari za Tanga na Mtwara au achague mwenyewe kutokana na uzoefu wake

Faith S Hilary said...

Ndio kile kile nilichosema kijijini kwangu...kuna mtu aliniambia kuwa wanataka "kuziba" yale matatizo waliyonayo ikifika kwenye international stuff(what are they called? congress? I have no idea) like these. At the end of the day, HOME SWEET HOME! :-D

John Mwaipopo said...

mnajua neo 'uwongo' liko ndani ya neno 'kiongozi'. hamana tabu wanayotuambia viongozi ni uwongo.