Saturday, December 19, 2009

Dunia ina mambo

Tukianza na huko Brazil, kuna mawili yaliyojiri wiki hii na "kunyanyua nyusi" za blogu hii. La kwanza ni la mwanadada-mwanamichezo m'beba vitu vizito Elizabeth Poblete raia wa Chile anayefanya mazozei nchini Brazil alipojifungua mtoto wa kiume wa miezi sita wakati akiwa mazoezini.
Mpaka wakati wa tukio, Elizabeth hakuwa na habari juu ya ujauzito wake na alikuwa akionekana "kujazia" na mwenyewe hakuwahi kuhisi lolote mpaka wiki moja kabla alipohisi mabadiliko kidogo tumboni. Siku ya tukio akiwa mazoezini alijisikia vibaya na kumpigia simu mtabibu wake na ndipo alipogundua kuwa yu-mjamzito. Hata hivyo alijifungua salama na yeye na mtoto kukimbizwa hospitali muda mfupi baadae. Unaweza kusoma habari kamili HAPA

Visit msnbc.com for breaking news, world news, and news about the economy


Pia hukohuko Brazil, mtoto wa miaka 2 amekutwa na zaidi ya sindano 40 mwilini ambaz zasemekana zilichomekwa moja moja na Babake wa kambo. Polisi wa nchini Brazil wamesema Baba huyo wa kambo aitwaye Roberto Carlos Magalhaes amekiri kufanya kitendo hicho kinachoshirikishwa na imani za kishirikina. Ifuate HAPA
Nako WISCONSIN nimekutana na hii ya kijana kuambiwa kuwa atahitaji RUHUSA YA KISHERIA kuwa na mahusiano ya kimapenzi baada ya kupatikana na hatia ya kuiba gari na kumtorosha mpenzi wake wa miaka 16.
Kijana huyo Jordan S. Christensen mwenye miaka 19, amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na uangalizi wa miaka 3 na katika kipindi chote hicho, hataruhusiwa kuwa na mahusiano bila ruhusa ya mshauri wake wa kisheria. Hii iko HAPA

6 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kali hizi

Ndekia said...

kaka nashukuru kwa mawazo yako na ushauri maana unanijenga sana nashukuru mkuu wangu kwa kuwa pamoja ila cha msingi inabidi ikiwezekana tuwasiliane zaidi e-mail yangu ni naza_ndekia@yahoo.com kwa mengi zaidi nashukuru kwa ushirikiano wako kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmmhh kazi ipo!!!

Mija Shija Sayi said...

Na mimi zimenishangaza sana hizi habari, ya huyo binti mnyanyua vizito nilikuwa sijaisikia mimi naona ndo raha ya kuwa active amezaa kiulaini sana mwenzetu, maana mmh!

Hope mtoto atakuwa salama.

Stay blessed.

Fadhy Mtanga said...

Kweli dunia ina mambo!

Faith S Hilary said...

Mmh...huyo wa mwanzo hajajua kama she was pregnant??? i heard it happens ila mmh...very weird...mtoto mwenye needles namuonea huruma mpaka basi...na wa mwisho i can only say..."mmh"t